Clemente Russo aliacha maumivu kwa Dontay Wilder na Oleksandr Usyk lakini wazoefu wangumi wa Uingeleza kwa kipindi kile walijiuliza “hivi imewezekanaje Russo amewapiga wote wawili”

Russo akitangazwa ubingwa baada ya pambano lake na Wilder

Russo ambae kwasasa ni afisa wa usalama nchini Italia, hakufanikiwa kabisa kuingia kwenye tasnia ya masumbwi kimataifa ila tayari ana medali mbili za Fedha za mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2007 na 2013 na taji la (WSB-World Series of Boxing Tournament).

Mwaka 2008 Wilder alishiriki tena Olimpiki katika jiji la Beijing  huku sasa akakutanishwa na Rakhim Chakhkiev  wa Urusi ambae nae bila huruma alimtwanga Wilder na kumfanya Wilder kuambulia medali ya Shaba.


Siku za karibuni katika mahojiano yake na chombo cha habari cha Skysport Wilder alisema “moyo wangu uliumia sana Olimpiki, unajifunza kwa miaka minne lakini ukiingia ulingoni mikono yako inaenda tofauti na ulicho dhamilia.”

Moja ya wachambuzi alisema “Wilder hakua bondia mzuri, alikua ana dunda dunda tu na ndio maana Russo anaweza kumpiga hata mara kumi katika mapambano kumi watakayo pamgiwa.

Wilder alizaliwa maeneo ya Tuscaloosa katika jimbo la Alabama, nchini mnamo mwaka 1985. Amepambana mapambano yake ya kimataifa 44,kushinda 42,matokeo ya sare 1 na la kupigwa moja lililochezwa mwanzoni mwa mwaka huu dhidi ya Tyson Furry. Pambano jilo lililopigwa tarehe 22 Februali lilimalizika kwa Wilder kupigwa kwa T.K.O na mpinzani wake Tyson Furry


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa