Klabu za Ujerumani kutoka ligi kubwa mbili wamekubali kuongeza katazo la mechi hadi Aprili 30 kwasababu ya Corona. Klabu zote 36 kutoka Bundesliga na Bundesliga 2 wanaangalia namna ya kufanya mechi zichezwe bila mashabiki.
Bodi ya Ligi ya Ujerumani imetangaza kutakuwa na timu ya madaktari na wataalamu kuhakikisha mfumo wa afya ya wachezaji kipindi mechi zitakaporejea.
“Tuna lengo la kumaliza ligi ifikapo Juni 30”, amesema Mkurugenzi Mtenadji, Christian Seifert.
“Kama mechi zitacheza, inamaana zitachezwa bila mashabiki, nadhani hata msimu ujao, labda mwisho mwa mwaka.”

Wiki iyopita Borussia Dortmund, Bayern Munich, RB Leipzig na Bayer Leverkusen walijiunga pamoja na kutoa 20 million euro kusaidia vilabu vyenye hali mbaya kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amesema; Ni bora msimu ungemalizika ili vilabu vipunguze anguko la kiuchumi.


Furahav
Corona noma