Lukaku Alivyomkosha Martinez

Mchezaji ambaye msimu uliopita alikuwa ndani ya klabu ya Manchester United na kuonekana uwezo wake umeshuka ikiwa ni tofauti na vile ilivyokuwa awali kwake alipokuwa katika klabu ya Everton, Lukaku amerejea katika kiwango chake na mwenye furaha kubwa sana ndani ya timu yake ya taifa.

Kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa, Martinez alisema tangu aanze kufanya kazi na nyota huyo amemuona kwa sasa akiwa na furaha ya aina yake na yupo huru zaidi ikiwa tofauti kabisa na vile ilivyokuwa awali. Kupitia hilo anaona ataweza kufaidika makubwa sana kutokana na namna ambavyo nyota huyo anaonekana kwa sasa.

Lukaku alikuwa nyota wa kwanza ambaye alisajiliwa na kikosi cha Inter Milan kwa kipindi cha hivi karibuni. Hiyo ikiwa ni tofauti na awali ambapo kikosi hicho kilikuwa na wachezaji ambao walikuwa wanapokea malipo ya kawaida kutoka katika kikosi hicho. Hiyo ni dalili njema ya maendeleo ya soka katika taifa hilo la Italia.

Usajili wake umeweza kugharimu kiasi cha £80m kutoka katika klabu ya Manchester United ambako alionekana kufanya mambo kinyume na matarajio ambayo klabu hiyo ilikuwa ikitegemea kutoka kwake. Hizo ni dalili za mapema kabisa kwa nyota huyo kuanza kufanya vizudi ndani ya klabu hiyo.

Nyota huyo mwenye miaka 26 alikuwa na mwanzo mzuri mara baada ya kufunga magoli mawili ya mapema kwenye michezo yake ya awali ya klabu hiyo katika ligi hiyo ya Italia. Huenda kukawa na mazuri zaidi kutoka kwa nyota huyo mara baada ya kuanza kushuhudia magoli ya mapema sana kwa uwezo wake.

Alizungumza hayo wakati wakiwa katika maandalizi ya mechi zao za kufuzu katika michuano ya Euro 2020 kocha huyo anaona kwamba katika maandalizi ya michezo yao amekuwa akimuona Lukaku akiwa katika hali tofauti lakini hii ya sasa ni kubwa zaidi kutokana na kumuona akiwa kwenye utayari na furaha kubwa sana.

Anaamini huu ni ukurasa mpya kwa nyota huyo ambaye anacheza soka lenye heshima ya aina yake. Kwa wakati huu ambapo soka limekuwa mchezo wa kimapinduzi sana anaona kabisa Lukaku akiwa ni kizazi kitakachokuwa na mafanikio makubwa kwenye soka kwa kipindi cha hivi karibuni.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.