Nyota wa Liverpool Sadio Mane ameweka bayana kuwa atakubaliana na uhalisia ikitoea Liverpool wakinyimwa taji msimu huu.
Mpaka viongozi wa Premier League wapo katika wakati mgumu wa kuamua namna ambavyo Ligi itaisha huku kila chaguo likionekana kuwa na changamoto yake. Wakati kukiwa na jitihada za kuhakikisha mechi zilizosalia zinachezwa ili kumpata mshindi wa taji hili, kumekuwa na taarifa za uwezekano wa msimu huu kubatilishwa.
Ikiwa msimu huu utabatilishwa basi jitihada za Liverpool katika kufukuzia taji hili ambalo wamelikosa kwa takribani miaka 30 sasa zitakuwa zimegonga mwamba, na watahitaji kuweka jitihada hizi katika msimu unaokuja.
Sadio Mane, akiwa mmoja wa wachezaji ambao wametoa mchango mkubwa sana kuhakikisha klabu ya Liverpool inapeta msimu huu ana wasi wasi na maamuzi yatakayofanyika kama ilivyo kwa wadau wengine wa soka, lakini yupo tayari kukubaliana na matokeo.
Sadio Mane na Mo Salah wamekuwa kama injini ya Liverpool wakitoa mchango mkubwa klabuni hapo. Mane ameona lango mara 14 katika mechi za Primier League msimu huu. Mane anasema kwa upande wake hawezi kujiona kama ni bingwa isipokuwa kama wataweza kupambania uwanjani kulipata taji hilo.

Mane anasema ilikuwa ni ndoto yake, na ndoto ya kila mwana Liverpool kushinda taji hili msimu huu. Lakini kulingana na athari ya virusi vya Corona kuna hofu kubwa ya kubatilisha msimu huu na hivyo kukosekana taji mwaka huu. Kwa mujibu wa Mane anaona suala hili limeleta athari sehemu nyingi na sekta nyingi mno huku watu wakipoteza maisha na wengine wapendwa wao, hivyo hawatakuwa na budi kukubaliana na hali.
“Naipenda kazi yangu, napenda soka. Nataka kushinda uwanjani. Nataka kushinda gemu na kupata taji, hicho ndiyo ninachopenda. Lakini kwa hali hii, chochote kitakachotokea nitaelewa. Imekuwa kazi sana kwa Liverpool, lakini imekuwa kipindi kigumu zaidi kwa mamilioni ya watu duniani. baathi wamepoteza familia na wamekuwa na hali ngumu zaidi. Lakini kwa upande wangu, ni ndoto yangu, nataka kushinda mwaka huu.”


Sylvester
Taji linastahili apewe Liverpool kivyovyote vile,iwe kwa League ikiendelea au kwa ushindi wa mezani