Wachezaji wengi wenye utajiri mkubwa duniani huupata kutokana na mikataba yao inayowajali na kuwafanya kuwa huru kufanya mambo mengi bila kuwa na mipaka; vilevile baadhi ya tuzo na nyongeza mbalimbali ndani ya mishahara yao na mikataba ya nje ya wadhamini mbaki mbali wanaowiwa kufanya uwekezaji wa matangazo kwa wachezaji wa aina yake. Baadhi ya wachezaji wanaoshikilia pesa ndefu kwa sass ni kama vile:
Cristiano Ronaldo
Utajiri wa Ronaldo unakadiriwa kuwa ni $450M kwa sasa na mapato yake yanatanuka mara kwa mara kutokana na mshahara wake ambao kabisa unafanya aweze kujaza kapu lake kadri siku zinavyozidi sogea mbele. Na mshahara wake unafika kiasi cha $61M ambacho sio kiasi cha mchezo kwa mchezaji kulipwa.
Lionel Messi
Kwa mshahara anaoupokea mchezaji huyo ilibidi azidi mapato ya Ronalo kwa kiasi fulani kwa sababu anapokea mshahara mzito zaidi yake; mshahara ambao ni zaidi ya $84M kitu ambacho ni mbali sana na kile cha mpinzani wake, Ronaldo. Lakini utajiri wake unasomeka $400M, kiwango hicho ni pamoja na mikataba ya kibiashara; hivyo alipaswa kuwa juu kabisa ya mwenzake.
Zlatan Ibrahimovic
Ni mchezaji mkongwe sana katika soka ambaye katika soka ameweka historia kubwa sana na anaendelea kufanya hivyo pamoja na umri wake kusonga mbele kidogo. Mbali na kuwa na vitega uchumi vinavyomfanya kuwa bora kiuchumi; pia ameweza kucheza katika vilabu vikubwa ikiwemo Juventus, Barcelona na Manchester United.
Wayne Rooney
Mchezaji wa Uingereza aliyestaafu kuichezea timu yake ya taifa kwa sasa. Anakadiriwa kuwa na utajiri wa $145M ambao ameupata katika maisha yake ya soka hadi sasa akiwa bado anacheza soka kuke Marekani. Mchezaji huyo wa zamani wa United amekuwa mchezaji wa kiingereza aliyefikia hatua kubwa sana kwenye soka kitu ambacho wachezaji wengi wanakitamani na heshima hiyo wanaitamani.
Neymar
Mchezaji huyo wa PSG kutokana na takwimu za Forbes anamzidi kwa kiasi fulani kimauzo Ronaldo lakini utajiri wake bado upo chini na unakadiriwa kuwa $140M. Utajiri wake anautengeneza kutokana na mikataba ya mauzo kibiashara na Nike pia na Dre beats.
Mbali na wachezaji hao pia wapo wengine kama Luis Suarez, Sergio Arguero.


Shani
Habari njema