Historia: Petr Cech na Makeke Yake

Mlinda mlango wa zamani wa Washika Bunduki wa nchini Uingereza, Petr Cech alipumzika kucheza soka akidai hana sababu ya kuendelea sana ili kuharibu historia zake. Katika hali ya kawaida mchezaji huyo anastaafu akiwa amefanya kila anachotakiwa kukifanya kama mlinda mlango, kwa kujenga historia kubwa ndani ya kikosi hicho na sehemu nyingine alizopita.

Mlinda mlango huyo alianza kufahamika zaidi katika ulimwengubwa soka alipokuwa ndani ya klabu ya Chelsea ambapo amekuwa klabuni hapo kwa kipindi kirefu sana na baadae kuona maisha ya pale yamemzoea akaamua kutafuta upinzani wa aina nyingine ndani ya klabu ya Arsenal. Ambapo napo bado alifanya kazi kubwa kitu kinachoendelea kumpa heshima hadi leo.

Amefanya kazi na makocha wenye historia pana sana kwenye ligi hiyo akiwemo Mourinho, Wenger ambao wamefanya naye kazi kwa kipindi kirefu; na kumwqmini mara zote kwa kumpa nafasi mara nyingi akiwa kama chaguo la kwanza. Kutokana na uwezo wake akiwa langoni, uhamasishaji na maamzi ya kiutu uzima akiwa uwanjani.

Amestaafu huko akiwa hadi sasa ametumikia soka ndani ya miaka 20 kutoka alipoanza kujihusisha na soka la ushindani zaidi. Ndani ya miaka hiyo amekwisha kaa kwenye milingoti mara 440. Hizo ni zile nafasi alizozipata akiwa pale darajani ambapo amekaa kwa kipindi kirefu sana pale Arsenal ambapo ndipo anatundika glovu zake akiwa amefikisha 36.

Akiwa langoni ni jitihada za pekee zinahitajika kumfunga mchezaji huyo, uimara wake na ujuzi wake katika soka utakumbuka sana na kila mwenye mapenzi ya dhati na soka. Maana amezuia hatari nyingi na kuzisaidia timu zao. Anekuwa muhimili mkubwa baada ya kwenda kuichezea Arsenal kwa muda uliobaki kwake.

Kipindi cha Mourinho alikuwa hakauki langoni, mechi karibu zote alikuwa anaomekana na helmeti yake golini akiwa anatoa michomo mingi ambayo ilimfanya yeye kama mchezaji kujenga historia na kuijengea historia klabu aliyopo, kitu ambacho ni ndoto ya kila mchezaji katika umri wake kufanya hayo.

Amecheza na majina makubwa mengi wakiwemo, Drogba ambaye kwa sasa ni mstaafu katika soka. Alijitwisha majukumu makubws ambayo yalikuwa ni chachu kwz timu yake wakati wowote. Ni aina ya wachezaji ambao wanastahili pongezi wakati wowote kutokana na mambo wanayoyafanya kuzisaidia timu zao.

Miaka yake 15 ndani ya Uingereza sio kitu cha mchezo kwa wachezaji, kwani wengi hupenda kuzunguka ligi mbalimbali ili kujionea tofauti zilizopo; na sio kusalia katika ligi ya aina moja tu. Ikumbukwe pia, kujitoa kwake uwanjani ndiko kulimpa majeraha ya muda mrefu katika kichwa chake hadi leo anavaa ulinzi ule kichwani: ili kujilinda na kuzuia majanga zaidi. Kwa sasa, amefanya maamzi sahihi katika wakati sahihi.

2 Komentara

    Hongera sana

    Jibu

    Uko sawa.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.