Klopp Alitabiri Hatma ya Safari ya Coutinho

Mchezaji Philippe Coutinho hali yake katika klabu ya Barcelona ilikuwa ipo katika hali ambayo haieleweki. Hii ni baada ya maisha yake ya kisoka ndani ya klabu hiyo kwenda nje ya kile alichokuwa akikifikiria kwa kipindi kirefu kwamba angejenga historia kwa kujiunga na klabu hiyo yenye historia kubwa katika soka.

Coutinho alijiunga na Barcelona mwezi Januari, 2018 akitokea Liverpool kwa uhamisho uliokuwa wa kihistoria ndani ya klabu hiyo. Aliondoka klabuni hapo akiwa na historia kubwa na rekodi ya aina yake ndani yake, lakini mambo yanaonekana tofauti kwa sasa; katika klabu yake hiyo mpya anayohudumu kwa sasa. Amekuwa ni mchezaji anayesugua benchi na kupata nafasi chache sana za kuonesha ubora wake uwanjani.

Maisha yake yakaendelea kukaa upande mbaya kutokana na ripoti zilizoendelea kwamba klabu hiyo ilikuwa ipo mbioni kumrejesha Mbrazil mwenzake, Neymar kutoka PSG kitu ambacho kingemkosesha namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho kutokana na nafasi za wachezaji hao uwanjani.

Haya yote yakiwa yanatokea, kocha wake wa zamani, Klopp aliwahi kumtahadharisha mchezaji juu ya tabia ya klabu hizo kubwa na tabia wanazowafanyia wachezaji wa aina yake. Kitu ambacho Coutinho hakuweza kukisikiliza kabisa na kuondoka klabuni hapo. Kitu ambacho hadi sasa kitakuwa kinamuumiza mchezaji huyo kutokana na kupuuza maneno aliyopewa na mwalimu wake hapo awali.

Baadhi ya vitu alivyowahi kumuambia mchezaji huyo ni kwamba, ni bora asalie klabuni hapo kwa sababu itamsaidia yeye kujenga jina lake na heshima ya timu anayochezea; kwenda katika klabu zenye majina kama Barcelona na Madrid kungemfanya mchezaji ndiyo lakini mwenye kuwajenga wachezaji wengine. Akiwa na maana atafanya kazi katika vivuli vya wachezaji wengine na thamani yake haiwezi kuonekana waziwazi. Maneno haya yanadhihirika sasa kutokana na hali anayopitia mchezaji huyo kwa sasa.

Mchezaji huyo alifanikiwa kuanza mechi tisa tu akiifungia timu hiyo magoli manne na kutoa pasi ya goli moja huku akiwa ameingia akitokea benchi mara saba. Takwimu hizi ni tofauti kabisa na zile alizowahi kuzipitia akiwa na klabu nyingine. Alikuwa zaidi mbadala badala ya kuwa mchezaji tegemezi katika timu. Hili ni suala ambalo mchezaji wa aina yake linaweza likachangia kushusha uwezo wake.

Pamoja na kutompa nafasi kubwa ya kuonesha makali yake lakini klabu hiyo bado ikawa ipo na ubora kitu ambacho ni dalili kwamba hawakuwa wategemezi sana wa huduma yake ndani ya kikosi hicho. Mbali na mchezaji huyo pia mchezaji mwenzake, Ousmane Dembele naye alikuwa yupo katika kipindi kigumu cha kuweza kudhihirisha ubora wake ili aweze kuaminiwa kikosini hapo kabla hajahamishiwa Ujerumani.

3 Komentara

    mwana kulitafuta mwana kulipata, angesikiliza wahenga yasingemupata#meridianbettz

    Jibu

    Sa itakuaje

    Jibu

    Duuh majanga kweli asiyesikia la mkuu huvunjika guu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.