Pirlo na Hadithi Zake

Bado naiwaza fainali ya world cup 2006, Pirlo wa usiku ule hakuwahi kuonekana kabla na hajawahi kuonekana tena. Usiku mmoja wa kiume sana katikati ya dimba. Wafaransa walilala wanaiota miguu yake. Waitaliano walilala wamekumbatia picha yake. Alikuwa kila kitu kwao. Aliitoa Italy kwenye miguu ya Gattuso na kuifikisha kwa Luca Toni. Alilimeza dimba lililokuwa na Vierra na Makelele .

Huyu ndiye Andrea Pirlo, kipindi anatoka Ac Millan kwenda Juventus Buffon alisema ” wakati Pirlo ananiambia anakuja Juve nilisema neno moja tu Mungu yupo, mchezaji wa kariba yake anakuja kwetu tena bure? Hamna cha zaidi ya kusema Mungu yupo.” Huyu ndiye Pirlo ambaye wahuni wa Turin walimuita “architect”. Alikuwa mbeba ramani wao pale Aliianz stadium☺.

Pale Millan wanamuita  il professore, kwa kindereko ni “the professor”. Mtaalam fulani wa kupiga pasi. Hajawahi kutokea binadamu kama yeye kwenye nyasi San Sirro. Angepiga pasi katikati ya watu sita alafu bado ikaenda kwa muhusika. Miguu yake ilikuwa na bikari, penseli, ruler na ufutio. Angetazama kulia alafu akaweka pasi kushoto.

Kipindi anajiunga na Ac Millan Ancelotti aliamini Pirlo ni deep lying playmaker, kiungo mkabaji anayehusika na ushambuliaji. Waitaliano walimuona Ancelotti kichaa, Ashakum si matusi. Unamchezesha vipi kiungo mkabaji huyu mtu ambaye hana nguvu miguuni? Waliuzoea mpira wa akina Demetrio Albertini na Roberto Donadoni. Walimuona Ancelotti mpumbavu, nilitangulia kusema Ashakum.

Wiki mbili tu walishampokea, wakasahau mpira wa kina Marco Tardeli, Pirlo aliwaaminisha kiungo mkabaji si lazima atumie nguvu. Kilichofuata ni stori tu, ndiyo huyu Pirlo tunayomzungumza mpaka leo.

Licha ya kutokuwa na kasi, nguvu na stamina atakumbukwa kwa uwezo wake kufanya interception. Atakumbukwa kwa uwezo wake wa kupiga free kick. Iwe kufunga au kuupeleka mojamoja kambani, alikuwa specialist wa hizo kazi. Kumbuka ile free kick kwake kwenda kwa Maldini kwenye ile fainali ya UEFA 2005, ile miracle of Istanbul. Absolute heavenly.

Vitabu vya historia vinadai ni kati ya wapigaji pasi bora kuwahi kutokea kwenye historia ya mpira. Saint Andrea Pirlo, the brain of Millan.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.