Moja ya Vituko vya Sarri!

Ni hulka ya binadamu kufanya mambo fulani ambayo mtu mwingine anaweza kutazama kwa jicho la tofauti na kuona labda jamaa akili zilimkimbia mara moja au inakuwaje! Meneja wa Juventus, Maurizio Sarri ameweka bayana baadhi ya mambo ambayo huyafanya, nimechukua kituko kimoja na kukusogezea hapa!

Moja ya Vituko vya Sarri,
Maurizio Sarri na Ronaldo: Juventus

Sarri alitumia mda mrefu sana kwenye ligi za madaraja ya chini kabla hajapata fursa ya kuingia kwenye ligi kubwa. Amesimulia kitu ambacho amewahi kukifanya akiwa anafundisha klabu iliyokuwa inashiriki michuano ya Eccellenza kule Tuscany.

Mwalimu huyu mkongwe anasema alikuwa na sehemu moja aliyopenda kupaki kupaki gari yake. Sehemu hii ilizoeleka na wachezaji kiasi cha kuanza kumtengenezea visa vya makusudi ili wamuudhi. Baadhi ya wachezaji walikuwa wanajaribu kuwahi kabla yake na kupaki sehemu anayoipenda.

Siku moja wakiwa na na mechi alifika na kukuta nafasi yake tayari imewekwa gari na mchezaji fulani, akakimbia chumba cha kubadilishia na kubwata kuwa “Aliyeweka gari kwenye sehemu yangu ana dakika tatu za kuliondoa”. Jama walikausha kama hawakusikia kitu.

Sarri baada ya kuona hivyo akawaambia kuwa sasa kama hakuna mtu anaenda kutoa yeye atatafuta njia nyingine mbadala! Unajua jamaa alifanya nini?

Sarri alienda kuendesha gari lake, akasukumia pembeni gari lililokuwepo hapo kwa gari lake! Kitendo hiki kilimuudhi mchezaji aliyepaki gari, lakini kwa sababu walishinda mechi kwa bao 2-0 furaha ya ushindi ilishinda lawama ambazo Sarri angezipokea!

Ukiacha hii, unakumbuka wewe umelia lini mara ya mwisho? Jana? Juzi? Basi Sarri pia, kama binadamu wengine yeye analia mara kibao tu. Ameweka wazi akizungumza na JTV kuwa hawezi kulia hadharani, lakini akiwa sehemu tulivu peke yake anamwaga kabisa machozi, anaamini siyo udhaifu, lakini ni namna unavyojitoa katika kazi fulani na mabo yakaenda tofauti.

2 Komentara

    Mzee wa mafegi. Ni Kocha mzuri anayesimamia anachoamini. Namukumbuka jinsi alivyomchezesha Ngolo Kante kama kiungo anayezuia mashambulizi ya adui toka juu badala ya mkata umeme ilivyozoeleka na hakubadilisha maamuzi pamoja na shutuma nyingi za mashabiki na wataalamu wa Soka#meridianbettz

    Jibu

    Sarri hakuna kocha hapo.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.