Nyota wa Liverpool Mohamed Salah ametoa maelfu ya tani za chakula na nyama safi kusaidia wakazi katika kijiji chake cha nyumbani kwao huko Misri wakati huu wa janga la coronavirus.
Salah alituma vifaa hivyo katika kijiji chake cha Nagrig, karibu na mji wa Basyoun kaskazini mwa nchi, na pia Alituma ushauri wa jinsi ya kujiweka salama. Kijiji hicho kina wakazi zaidi ya 8500.
Baba wa mchezaji Huyo, Salah Ghaly, aliliambia gazeti la Al-Masry Al-Youm kwamba mtoto wake anatamani afya na usalama wa kijiji hicho, huku akiwataka wakazi waache mikutano mikubwa.

Aliongeza kuwa kijiji kimepatiwa Sanitizer na masks ambazo zinatarajia kusambazwa kwa wakazi kwa nia ya kupambana na kuenea kwa COVID-19, ambavyo vimesababisha vifo vya watu 205 nchini Misri.
Baba yake huyo aliongezea kuwa ng’ombe wawili watachinjwa na nyama hiyo itapelekwa kwa watu wa Nagrig na vijiji vinavyozunguka eneo hilo.
Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah alichapisha video ya Instagram akifanya mazoezi binafsi ambako yupo kizuizini nyumbani kwao akisubiri kuanza tena kwa soka huko England. Salah, ni kama wachezaji wote wa Premier League, wamekuwa wakijaribu kujifua ili kutunza viwango vyao na kuweka afya zao sawa..


Salma
Jambo zuri
Mariam mtandama
Mambo mazur