Mlinzi wa Barcelona, Samuel Umtiti ameingia kwenye kipaumbele cha Napoli kama mbadala wa Kalidou Koulibaly ikiwa klabu itamuuza.
Kuna ripoti kibao kuwa Kalidou Koulibaly anataka kusepa Stadio San Paolo msimu huu wa joto, na hivyo tayari klabu nyingi zikiwemo Real Madrid, Manchester United na Paris Saint Germain zimeonesha nia ya kutakla kumsajili.
Bila shaka Napoli wanahitaji mbadala wa kuziba pengo litakalo achwa na Koulibaly, na kwa mujibu wa ripoti Umtiti ndiye nyota pekee ambaye amefikiriwa kupewa kipaumbele zaidi na klabu hii.
Nyota huyu ana miaka 26 na raia wa Ufaransa, alisajiliwa kutokea klabu ya Olympique Lyonnais mwaka 2016 kwa dau la paundi milioni 25. Dau la staa huyu kwa sasa linatajwa kuwa paindi milioni 50.
Hata hivyo inahofiwa kuwa staa huyu anweza kuuzwa kwa dau dogo zaidi kwa sababu ya changamoto ya kiuchumi iliyoletwa na janga la covid19 amabayo imepelekea kushuka kwa ada za wachezaji Ulaya.
Hata hivyo, Umtiti hajawa na msimu mzuri sana mwaka huu baada ya kupata changamoto mara kadhaa za majeraha akiwa amecheza mechi 16 tu msimu huu akiwa na Barcelona.
Man United wanafikiria kuwa Umtiti anaweza kuwa mbadala wa Koulibaly ambaye atawagharibu karibu paundi milioni 100.


Daniel
He should come to the premier league
Povel
Habar njema