Nyota wa zamani wa Liverpool, ambaye pia amewahi kuchezea klabu za Manchester City na Brighton, Michael Robinson amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.
Staa huyu wa zamani pia alikuwa akifanya kazi kama mtangazaji na mchambuzi wa soka baada ya kumaliza kucheza soka la kulipwa.
Chapisho kupitia akaunti ya Robinson ya Twitter lilitoa taarifa ya kifo chake. Familia ya Michael Robinson imetumia akaunti hii kuuleza umma namna walivyofikwa na huzuni baada ya kumpoteza mpendwa wao na kushukuru wapenzi na mashabiki waliokuwa wakimpa sapoti na kumuonesha mapenzi nyota huyu wa zamani kwa kipindi chote.
Michael ambaye amecheza mechi 24 kwa nchi ya Jamhuri ya Ireland, alichezea klabu nyingine pia za Preston, QPR na Osasuna.
Baadhi ya vilabu ambavyo Michael Robinson aliwahi kuchezea tayari wameshaonesha kushiriki katika msiba huu, na kuungana na familia ya staa wa zamani wa Liverpool, Manchester City, na Brighton.
Liverpool wamechapisha katika mitandao yao ya kijamii andiko linalosomeka kuwa: ”
Tumehuzunishwa sana na kifo cha mchezaji wetu wa zamani Michael Robinson, akiwa na umri wa miaka 61.”
“Mawazo ya kila mmoja wetu hapa klabu ya Liverpool yapo pamoja na familia ya Michael na marafiki katika kipindi hiki kigumu”
Pumzika kwa amani, Michael”.
Chapisho la Maombolezo la Liverpool
We’re deeply saddened by the passing of former player Michael Robinson, aged 61.
The thoughts of everybody at Liverpool Football Club are with Michael’s family and friends at this sad time.
Rest in peace, Michael. pic.twitter.com/o8Zu3hjICc
— Liverpool FC (at 🏠) (@LFC) April 28, 2020


Frank patrick
Rest Easy Kop
Gabriel
Habar njema sana 👍
farida ahmadi
R.i.p