
Ila hiyo ni heshima ya nje uwanja tu hali ilikuwa tofauti kabisa uwanjani. Lampard alikuwa ugenini leo, kimbinu alidhaniwa angejihami zaidi, afunge uwanja, asifunguke kabisa. Ila haikuwa hivo alikuja hapa anajiamini sana, akaonesha wazi anataka pointi zote tatu, akaanza na mabeki watatu.. ujasiri wa hali ya juu sana. Unajiamini vipi kuanza na defenders watatu ukicheza na mou ugenini? Ila Lampard ni kati yale wanafunzi wasiosahau mafundisho ya waalimu wao. Alikuja akijua Mwalimu wake anatumia notes zilezile alizokuwa anatumia miaka 15 iliyopita. Alijua alichobadilisha mou ni timu tu, ila mbinu ni zilezile alizozitumia 2004. Hivo hakuihitaji sana kuupigia msuli mtihani wa leo. Alijua tu kumbukumbu zake zinamtosha kabisa kufaulu. Na ndicho alichokifanya. Kukumbuka tu namna walivokuwa wanacheza na timu zinazimiliki mpira kipindi cha Mourinho. Akajua wazi na leo atakuja hivohivo. .
Alipoweka kumbukumbu zake sawa kikabaki kitu kimoja tu, kutafuta majibu mapya kwa kutumia homework waliyoachiwa zamani. Alipoyapata akawapa wanafunzi wake, ikabaki tu kwenda kufaulu.
Alijua wazi Mou ataanza na wakabaji sita ili awanyime nafasi kwenye tatu ya mwisho ya uwanja. Awaache waufurahie mpira alafu awaadhibu kwa counter attack. Lampard akatumia nafasi hiyo ya kumiliki mpira, ila akawajaza katikati kuziba mianya ya pasi ndefu, akamtawala mwalimu wake jumlajumla.
Alikumbuka tabia ya mwalimu wake kuwafanyia man marking baadhi ya key players kwenye mechi kama hizi. Alichokifanya yeye akaweka benchi. Na ndiyo sababu ya Pulisic na Jorginho kuanza kwenye mbao leo. Mwalimu akatumbukia kwenye mtego wa mwanafunzi kwa kukosa aliotarajia kuwafanyia marking.


SADICK
Ilikuwa game nzuri sana!
Abram
Sema ukiachana nayote Mourinho ni kocha mwenye mbiflani za kushinda mi nakubali uwezo wake.
farida ahmadi
Kweli kabisah Mourinho ni kocha mzuri Sana ambaye pia hanajituma vizuri kufundisha kikosi chake