Timo Werner ametangaza kuwa anapendelea kuhamia kwenye ligi nyingine baada ya kuthibitisha kuwa hana nia ya kujiunga na Bayern Munich.
Ripoti nchini Ujerumani wiki hii zilidai nyota huyo wa RB Leipzig alikuwa ameamua kupiga chini ofa Bayern, akisisitiza ni bora kuhama Bundesliga na kutua klabu nyingine kuliko kubakia Ligi hiyo hiyo na kujiunga na klabu tofauti.

Werner, ambaye ameripotiwa kupokea ofa kutoka Chelsea na Manchester United, ana kifungu cha uhamisho kwenye Mkataba wake cha pauni milioni 50 na anapendelea kujiunga na Liverpool kwenye dirisha linalofuata la uhamisho. Werner alisema: “Changamoto kwenye ligi ya nje ingenivutia badala ya kuhamia Bayern.”
Chelsea na United pia wanamsaka mshambuliaji huyo, lakini wanajua kuwa Liverpool ndio wanaongoza mbio hizo za kuwania saini yake. Werner amejidhihirisha kama mmoja wa Washambuliaji hatari zaidi barani Ulaya, akiwa na magoli 27 katika mashindano yote kwa klabu yake ya Leipzig msimu huu.


Kenani
Hyo ni jesh awez kutoka hapo
Furahav
Bora uende man u mzee baba.
Gabriel
Amengalia mbal ukiangalia England ndo lig inayopendwa dunian
Samira
Ameangalia mbali zaidi hili akarisakate soka England
Hamidu
Yupo vzr..anatakiwa aje man utd
Nasra
England panakufaa
Zainabu
England mbona pazuri tu we hamia
Aziza moshi
Bora uende tu uko England
Ibrah
Kaangalia pesa na ligi bora
Ester jackson
Aangalie masilahi na asiache kujituma
Shafii
Jamaa anajua Sana kufumania nyavu ni bora aje EPL pale aje kuleta chachu ya magoli England
John mwakalosi
Ana gut za kukataa offer ya munich kweli
felister
👍
Ester mmakasa
Kubadili mazingira ni Jambo la msingi sana hata Mimi nitafurahi kama Werner atahamia ligi nyingine
SADICK
Tunamukaribisha Stamford Bridge
mathayo sonje
nenda England ligi yenye ushindani dunian
Neema juma
Aje tu
Neema hassan
Mashabiki wa man utd tunamsubiri kwa hamu..
Asia Abdy
Maslah muhim
Waziri
Huyu anataka kufanya kazina klop alishawai kusema
Evaluziga
Angalia maslahi mzee babaeeel
Schola
Mfanyakazi hanaonekana tu
Mariam mtandama
👌
Adelta
Tunamkaribisha sana
Theckla
Tunasubiri
Khadija
Bola aende man#meridianbettz