Arsenal, Tottenham na Borussia Dortmund zaingia vitani kuwinda saini ya kiungo wa kati wa Flamengo Gerson, baba wa nyota huyo wa Brazil amethibitisha.Gerson alifanikiwa kuonesha kwangi kikubwan sana kwenye fainali ya klabu bingwa duniani ambapo Flamengo walikutana na Timu ya Liverpool ambao ndio mabingwa wa ulaya.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hakuwa na msimu mzuri alipojiunga na Roma (2016) lakini amekuwa mchezaji muhimu kwa Flamengo tangu arudi nchini Brazil, lakini maekua akitazamwa sana na vilabu vikubwa ulaya.
Gerson amecheza Flamengo michezo 43 tangu arudi nchini Brazil na amefanikiwa kutajwa kwenye timu bora ya mwaka Serie kutokana na mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo kutwaa taji la ligi na Ligi ya mabingwa (CopaLibertadores) mwaka 2019.
Baba mzazi wa nyota huyo mzee Marcos Santos, ambaye pia ni meneja wa Gerson, amesema:
“Hakuna mtu aliyejua kuhusu Arsenal kumtaka Gerson, lakini kwa kuwa sasa ninawaambia, kila mtu amejua,”
Juu ya taarifa ya Spurs na Dortmund, ameongezea kwa kusema: “Kila unalosikia kuna ukweli, vilabu hivyo vimekuwa vikimfatilia.”


christopher
Watu wa namna hii wanakuwaga hyped sana na medias ila wakisajiliwa tu kwenye klabu kubwa viwango vyao ndo vinaishia hapo, wamepita weng kama hao, ila labda huyu atakuwa wa tofauti
Gabriel
Gerson anajua
Lombo
piga kaz dogo
Emmy cleopa
Gerson ni fundi sana
Adelta
Gerson namkubal Sana
Frank patrick
Epl ataiwezaa?
Shafii
Asibweteke kwa kuona vilabu vikubwa vinamuhitaji akapambane afike mbali
Furahav
Vijana ndo kila kitu.
Genia Sikaluzwe
Gerson fundiii Sana wa mpira
Fatina mfingi
Gerson yupo vizur