Guardiola Atarejea Barcelona?

Klabu ya Barcelona inamtaka Guardiola kurejea klabuni hapo! Mkataba wa sasa wa Guardiola na klabu ya Manchester City unaisha mwezi Juni 2021.

Guardiola amekuwa akihusishwa na kurejea klabuni Barcelona, na sasa Joan Laporta ambaye anatarajia kuwania nafasi ya raisi wa klabu ameweka wazi nia yake ya kutaka kumrejesha Pep Guardiola kutoka ligi ya Uingereza!

Laporta alishawahi kuwa raisi wa Barcelona mwaka 2003 hadi mwaka 2010, kipindi ambacho Guardiola alipandishwa hadhi kutoka timu ya vijana mpaka kufundisha timu ya watu wazima, mwaka 2008.

Laporta ametangaza nia ya kuwania uraisi wa klabu hiyo, na katika kitu anachokifikiria kuwafanyIa barcelona ni kumrejesha meneja amabaye amepata mafanikio makubwa katika soka kwa sasa, Guardiola.

Josep Bartomeu, raisi wa sasa wa Barcelona anaachia kijiti msimu ujao wa joto, na mchakato wa kumpata mrithi wake unaendelea.

Kwa upande wa Guardiola, ambaye mkataba wake unaisha Juni 2021, hatma yake imeendelea kuingia ukungu baada ya Man Cityn kupewa adhabu kwa kuvunja sheria ya UEFA ya manunuzi (kesi ambayo wameikatia rufaa)

Baada ya kuteuliwa na Laporta pale Barcelona, Guardiola alipata mafanikio kadhaa, akifanikiwa kushinda mataji matatu ya ligi na mawili ya ligi ya Mabingwa 2009 na 2011.

Pep Guardiola Atarejea Barcelona?
Pep Guardiola akisherekea moja ya mafaniko yake Barcelona: 2009

 

Katika kutangaza nia yake ya uraisi, alizungumzia mambo kadhaa kuhusu Guardiola

“Nitafurahi sana kurejea kwa Pep Guardiola, lakini yupo City sasa na ni uamuzi ambao atatakiwa kuufanya. Amekuwa ni mfano wa kila mtu anayehusika na Barcelona nafikiri mashabiki wengi watafurahia sana kama akirejea kuifundisha klabu tena.”

Barcelona wakiwa Chini ya Guardiola

3 – La Liga (2008-09, 2009-10, 2010-11)

2 – Ligi ya Mabingwa (2008-09, 2010-11)

2 – Copa del Rey (2008-09, 2011-12)

2 – Kombe la Dunia la Vilabu (2009, 2011)

2 – UEFA Super Cup (2009, 2011)

3 – Spanish Super Cup (2009, 2010, 2011)

45 Komentara

    Duuuh! Habar mpya

    Jibu

    dah iko poa iyo

    Jibu

    Hiyo ni habari njema sana

    Jibu

    Ni habari nzuri

    Jibu

    Asanten meridianbet kwa taarifa

    Jibu

    Akireje utakuwa ni vizuri Sana

    Jibu

    Barcelona wanazidi kuongea nguvu kwenye klabu yao wafanye wamchukue tu

    Jibu

    Itapendeza

    Jibu

    Akirejea itapendeza sana

    Jibu

    Namkubar Sana uyo jamaa.arud tu

    Jibu

    Ni jambo zuri sema tu nawasisi juu ya kizazi kilichobaki Barca kama kitarudisha heshima yake.

    Jibu

    Iko poa sana

    Jibu

    Asante meridian kwa taarifa

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Kocha bora.

    Jibu

    Itakua poa Sana akirejea Barcelona

    Jibu

    👌👌👌👌

    Jibu

    Coach bora muda wote anayejua kutengeneza timu yake. Akirudi barca atasumbua

    Jibu

    Habari Safi sn

    Jibu

    Ni vizuri

    Jibu

    Nihabari njema

    Jibu

    Guadriola kocha bora na ataweza kurudisha heshima ya Barcelona kama zamani…chaguo zuri

    Jibu

    Ni vizuriii pia #meridianbet.

    Jibu

    Akirejea hatakuwa na makali yale aliyokuwa nayo hapo awali sio chaguo zuri

    Jibu

    Akifanya hivyo itakuwa poa

    Jibu

    Hasirud Tena kwn ni mmoja aliyeweka heshima kwa kucheza na kufundisha klabu hyo mm natumain kwamb akirud hataaribu sifa zake Asante meridian bet# meridian bet#

    Jibu

    barcelona wako vizuri kwa kuongeza jembe

    Jibu

    Karibu sana Barcelona

    Jibu

    Guadiola ni kocha mzuri

    Jibu

    Safi sana kocha mzuri uyo

    Jibu

    Me sizani Kama nijambo jema kurudi baka kwa sababu amekaa pale muda mrefu pia ametoka na heshima so anaweza akarudi alafu asiifikishe timu inapotakiwa akawa amevunja heshima yake#meridianbettz

    Jibu

    Namtabilia kufanya vibaya akirejea tena

    Jibu

    Asanteee meridian kwa taarifa

    Jibu

    Iko poa Sana #meridianbet

    Jibu

    Pep is successful football Manager. Thanks #MeridianbetTZ

    Jibu

    itakuwa safi sana kama atarejea tena

    Jibu

    Hii ni habari njema kwa Guardiola

    Jibu

    Sidhn km itawezekana ngoja tuone

    Jibu

    Chaguo zuri sana kwa barcelona

    Jibu

    ni jambo nzuri kwa mashabiki wa barcelona

    Jibu

    Nijambo zuri

    Jibu

    Duuh asiende abaki man city

    Jibu

    Habari nzuri Sana na njema pia hata mashabiki wake na wachezaji wake watafurahia

    Jibu

    Itakuwa poa sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.