Jana kulikuwa na gemu kali sana ya Berlin derby iliyofungua mechiwiki ya 27 ya mashindano ya ligi kuu ya nchini Ujerumani, Bundesliga, ambayo ilirejea tangu wiki iliyopita baada ya kwenda likizo ya lazima.
Hapa ninakuletea mambo muhimu ya kuyatazama sana mwishoni mwa wiki hii katika ligi hiyo. Usisahau kuwa bado unaweza kuzibetia gemu hizo zote hapa hapa na kushinda sana ukiwa nasi.
Ligi hiyo ya Bundesliga inaendelea tena wikiendi hii ikiwa ni muda wa mechiwiki ya 27 kwa sasa na imeanza rasmi jana usiku kukiwa na gemu nzuri sana iliyotoa burudani ya aina yake uwanjani.
Hata hivyo hayo yameshapita, vipi tena leo?
Mbio za top four: Monchengladbach v Leverkusen
Wawili hawa wako katika hali nzuri sana kisoka na wanakutana leo Jumamosi wakiwa wanawania nafasi ya kuingia kwenye nne bora ya ligi yao. Borussia Monchengladbach wanakamatia nafasi ya tatu wakati hawa Bayer Leverkusen wanakalia nafasi ya tano wakiwa na jumla ya alama 50 mpaka sasa, wako alama mbili nyuma ya wapinzani wao wa leo.
Wote hawa wameshinda gemu zao zilizopita lakini hali ya Gladbach awapo nyumbani huwa ni faida kubwa sana kwao. Zaidi ya hayo, Monchengladbach wameshinda mechi zao mbili zilizopita walipokutana pamoja uwanjani. Itashangaza sana kuona kwamba wamewapiga wenyeji wao ambao ni upande wa Peter Bosz wakiwa kwao mara moja pekee katika gemu zao nane zilizopita.
Hatari zaidi pale mkiani
Hawa akina Paderborn na Werder Bremen wapo katika uzi mwembamba sana wa kuharibikiwa mambo yao kwa sasa. Jamaa hawa wawili wanakamatia nafasi mbili za mkiani mwa msimamo wa ligi ya Bundesliga wakiwa na jumla ya mechi nane pekee ili kumaliza msimu huu.
Walio chini zaidi, Paderborn hawajashinda mechi yao yoyote katika gemu zao saba zilizopita kwenye ligi. Wamepoteza mechi tano kati ya hizo. Wakati huo huo, nao Bremen wapo katika msukosuko sana kwa sasa. Mabingwa wa zamani wa Bundesliga wameshinda mechi mbili pekee kati ya sasa na mwezi wa Septemba kwenye ligi yao.
Wamepoteza mechi sita katika mechi zao saba walizocheza. Paderborn anakuwa mwenyeji wa Hoffenheim wakati nao Bremen wanawatembelea wale walio katika nafasi sita za juu, Freiburg. Endapo mfumo wao ukiendelea kuwa sawa na wakati uliopita mambo yanaonekana kuwa mabaya kwa jamaa wote hao.
Bayern na msiba zaidi kwa Frankfurt
Bayern wanarudi uwanjani wakiwa wameshinda mechi yao dhidi ya Union Berlin. Wanatazamia kuimarisha hali yao ya kimchezo wakiwa pale kileleni wakati wanakutana na Frankfurt siku ya leo Jumamosi katika gemu ya jioni kabisa mwa siku.

Hao Frankfurt wapo katika hali mbaya sana kwa sasa. Jitihada zao za kurudi katika mstari zinaonekana kuwa ni majanga zaidi kwao kwani wamekuwa na mafanikio machache sana. Wamepoteza gemu kwa 3-1 walipokutana na Monchengladbach na kuwafanya wawe wamepoteza mechi nne mfululizo katika ligi yao ya Ujerumani.
Wanakalia nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi wakiwa na alama tano kuelekea kwenye hatari ya kushuka daraja. Nao Bayern wameshinda mechi zao 11 kati ya mechi 12 walizocheza kwenye ligi, hivyo hawa akina Frankfurt wana kazi nzito na wajipange sana.


winfrida
game ilikuwa kali sana
frank patrick
Kama naona Dortmund anapoteza leo hivii
Ester mmakasa
Hiyo ni safii sana kwa kutujuza habari za muhumu kama hizi.
Salma
Wakaze buti
Hamidu
Safi kwa dondoo nzuri za kimichezoo.# meridianbettz.
Gabriel
Jamv leo litakuwa poa
Juliana
Kweli inabidi wajipange, maana ngoma nzito.
Furahav
Mchezo mkali sana.
mwakalosi
huu mchezo unaweza ukawa na gg tu
David pere
Ya leo Ndio ngumu kuelezeka kabisa maana wote ni mafundi
Lombo
mmh
Povel
Ilikuwah bonge la derby thanks meridian kwa update
dorophina
Mechi ilikuwa ya kibabe sana
Genia Sikaluzwe
Mechi ilikuwa Kali sana
Hope mwaikuka
Kaz kaz
Carolyne
Itakua hatariii
felister
hii game ya Leo itakua ngumu sana
Warda
Maskini Frankfurt nawapenda#Meridianbettz
Ernest
Buyern atapata tena ushindi mwembamba
Zeiyana iddi
Litakua bonge la mechi
aisha
Kazi kazi
Khadija
itakuwa bonge la mechi#meridianbettz
SADICK
Nahisi mechi zote kuwa na magoli mengi #Meridianbettz
Christopher
#Bundesliga , #meridianbet ngoja tuone na leo
Neema juma
Itakuwa bongee la mechiii.za kibabeee
Theckla
Ilikuwa bab kubwa Asante kwa mrejesho
Mariam mtandama
Duuuh
Emmy cleopa
Hatari sana
Genia Sikaluzwe
Bayern Munich ushindi upo
Lydia Emmanuel Magoti
Hii mechi ilikuwa atarii sana
Fatina mfingi
Mechi ilikuwa si mchezo