Wasiwasi wa Guardiola Kumkosa Aguero

Pep Guardiola ana wasiwasi kuwa Sergio Aguero anaweza kuikosa sehemu yote ya msimu iliyobakia baada ya kupata jeraha la goti.

Mshambuliaji huyu wa Manchester City ni mmoja ya wanaopigiwa upatu wa kutwaa Kiatu cha Dhahabu msimu huu, lakini hili linaweza kumkwamisha.

Aguero yupo nyuma kwa magoli matatu tu dhidi ya Jamie Vardy katika kufukuzia Kiatu cha pili cha dhahabu.

Aguero alipata jeraha la goti kwenye mechi ya Manchester City dhidi ya Burnley. Tangia alipopata taarifa hizo, Guardiola alionekana kuwa na simanzi.

Wasiwasi wa Guardiola Kumkosa Aguero
Sergio Aguero

Wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa hanari, Bosi huyu wa City alisema kuwa ilikuwa ni taarifa mbaya. Na alisema kuwa Aguero amekuwa akipambana na shida ya goti kwa miezi kadhaa, hivyo kwa sasa hali siyo nzuri.

Taarifa zinasema kuwa anatarajiwa kuikosa mechi dhidi ya Chelsea Alhamisi. Guardiola anasema ana wasi wasi kama anaweza kukosa msimu mzima, lakini madaktari wanaweza kuzungumzia hilo vyema zaidi. Ni matumaini yake hali itakuwa si mbaya sana.

Kwa sasa Sergio Aguero ndiye anaongoza kwa magoli Man City katika michuano yote akiwa na magoli 23, na magoli 16 ya ligi pekee, magoli mawili zaidi ya Raheem Sterling.

60 Komentara

    Daaaa pole yake Sidhani Kama Atapata kiatu cha Dhahabu#Meridianbettz

    Jibu

    Kutokana na majibu ya madaktari wanavyosema kuwa hali yake imeanza kukaa sawa.inawezekana akacheza

    Jibu

    Staa huyo wa argentina ndio mfungaji wa klabu ya manchester city mara zote na kuwania kiatu cha dhahabu ila msimu huu kwake sio mzuri kwa majera aliyokuwa nayo staa huyo pole aguero pia pole nyingine kukosa kiatu cha dhahabu maana jamie vardy ndio furaha yake wwe kuwa nje kwenye game zilizo salia

    Jibu

    Jamani pole sana kaka lakini pia usijali afya ndio kitu cha msingi

    Jibu

    aguero majeraha yanamuandama sana guardiola inabidi ahakikishe madaktari wanamuweka sawa aweze kucheza msimu mzima

    Jibu

    Pole sana ilikuwa mda wako mzuri sana wa kumalizia mechi zilizo baki sasa wamepata nafasi watu wengine pole sana

    Jibu

    Asiwe na wasiwasi atapona tu

    Jibu

    Hawawezi kutetereka hata Kama watamkosa aguero wachezaji wengine wapo

    Jibu

    Afya ni bora kuliko kitu chochote

    Jibu

    Nanavyo mkubali sijui itakuwaje

    Jibu

    Aguero pole yke Sana, inabid akae benchi kwa msimu huku madaktar wakiendelea kuchek afy yke.

    Jibu

    Apa anayefukuzana naye katika kuwania kiatu cha dhahabu ndo muda wa kufanya mapinduzi

    Jibu

    Kun Sergio aguero polen sn tukutane next season thnks meridian bet tz kwa update

    Jibu

    Aguero ni mchezaji mzuri ila kwa man city wanakikosi kipana haitakua tatizo sana

    Jibu

    Ni jambo la kusikitisha sana kwa kiungo huyo kwan kupata jeraha kwake kumekuwa mtihan mkubwa sana kwa club yake na like mfanya pepe guardiola awe na huzun sana kwa mshambuliaji wake na kutammfanya sterling achukue kiatu ila club ya man city pia haitokuwa sawa kutokana na kumkosa aguero mechi ijayo kwa upande wng naona watakuwa na kibarua kigumu kwan aguero n mshambuliaji mzur sana had muda huu ana magol 23 hivyo anachokiz guardiola yuko sahihi
    # meridianBetTZ

    Jibu

    Pole ila ucijali utapona

    Jibu

    Lazima awe na hofu maana ni mchezaji tegemezi

    Jibu

    Mimi ninakuombea upone haraka aguero kiatu tukichukue

    Jibu

    Aguero pole ila ucjali utapona

    Jibu

    Pole yake atapona

    Jibu

    Pep guardiola anajua umuhimu wa sergio aguero maana sio kwa kuumia na kukosa kiatu tuu hata makali ya safu ya ushambuliaji itapungua ukalibu na kama kweli msimu huu uliobak atakua nje basi ndio muda wa jamie vardy kufanya yake ila kwa staa huyu wa argentina mkwe wa maradona ni mchezaj mkali sana pale epl na n mfungaji wa man city wa misimu yote pale Etihad sasa pia na umri unaanza kumtupa mkono sasa pep bdio muda wa kuanza kuwa kuweka iman kwa kina gabriel jesus na kuwapika vya kutosha

    Jibu

    Duuh majanga

    Jibu

    Tatizo ilo tayari ila anaefukuzana nae atapata tu

    Jibu

    Lakini majibu ya daktari yanaleta matumaini

    Jibu

    Maskini mungu ampiganie ili apone na maisha mengine yaendelee.

    Jibu

    Namkubali sana

    Jibu

    Maoni: Duuuh pole sana Sergio Aguero

    Jibu

    Yupo sahihi lakini wajipe moyo

    Jibu

    Pole yake
    Asijali afya Ni kila kitu mpira upo tu

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Polee

    Jibu

    Mungu akusaidie upone haraka

    Jibu

    Changamoto za mpira huja pale mchezaji anapo pata amajeraha now Pepe Ana shida kwenye timu yake kukosa mchezaji muhimu
    # meridianBetTZ

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Ni pengo la man city

    Jibu

    Dah ni habar mbaya Kwa mashabik wa city pia kwake maan yamezma ndoto za yeye kuja kuwa mfungaji bola

    Jibu

    Litakua pengo kubwa Sana kwa man city

    Jibu

    Maoni:pole yake jamani

    Jibu

    hizo ni changoto to za mpira wengine wapo

    Jibu

    Kwa man city ni mchezaji muhimu Kama watamkosa itakuwapengo kubwa sana

    Jibu

    Duh majanga

    Jibu

    Atakaa sawa tu

    Jibu

    Pole sana.atakuwa sawa tu

    Jibu

    sidhani kama ataweza kurudi mapema maana madaktari hawajayoa report kamili na itabidi asafiri hadi jiji la barcelona kupata matibabu

    Jibu

    pole sana atakaa sawa tuu#meridianbettz

    Jibu

    Aisee majanga

    Jibu

    Atapona tu asijali..

    Jibu

    Habari mbaya kwa man city

    Jibu

    Atakaa sawa tuu

    Jibu

    Hakika atapona na atakuwa sawa tuuu..kama ipo ipo tuuu kiatu atakipata vizuri

    Jibu

    Atapona na atafanya kazi yake asijali sana Pep

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Dah inasikitisha Sana lakini gardiola asikate tamaa kabisah kwani hatapata tyuu mchezaji mzuri Sana hivyo afya ni kitu muhimu Sana kuondoka kwa Aguero sio kwamba ndio mwisho wa Manchester city hivyo asikate tamaa pengo lake litazibwa tyuu

    Jibu

    Pamoja na Aguero kuumia bado Man City wana mbadala,pengo lake halitaathiri timu#meridianbettz

    Jibu

    Sad news

    Jibu

    Pole Sana Ila ahsante kwa taarifa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.