Chelsea Walivyozidi Kuwadidimiza Aston Villa!

Ushindi wa ugenini wa magoli mawili kwa moja, dimbani Villa Park umewahakikishia Chelsea kusalia salama katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo huku wakiwa na alama tano zaidi ya Manchester United wanaoshika nafasi ya nne.

Magoli mawili ya Christian Pulisic na Olivier Giroud yaliwahakikishia usalama vijana hao wa Frank Lampard katika nafasi ya nne huku yakiongeza matumaini yao ya kushiriki Champions League msimu ujao.

Matokeo hayo, kwa upande mwingine yamezidi kudidimiza juhudi za Aston Villa ambao wanapigania kubaki katika ligi kuu msimu huu. Ilikuwa ni nafasi nzuri kwa timu hiyo kujiondoa katika hatari ya kushuka daraja hasa baada ya timu za West Ham na Bournemouth ambazo nazo zinapambana kubaki ligi kuu kupoteza katika michezo yake ya Jumamosi.

Aston Villa walikuwa wa kwanza kupata goli katika mchezo huo. Goli hilo lilifungwa na Kortney Hause katika dakika ya 42 tu ya mchezo na kuwafanya waende mapumziko wakiwa kifua mbele.

Hata hivyo bahati haikuwa upande wao kwani Chelsea walitumia vizuri udhaifu wa Aston Villa wa kujilinda zaidi kuliko kushambulia kuwaadhibu.

Kwa matokeo hayo, Chelsea wanazidi kujiwekea mizizi katika nafasi ya nne wakiwa na alama zao 51 huku Aston Villa wakishuka mpaka nafasi ya 19 wakiwa wamejikusanyia alama 26 katika jumla ya michezo 30!

60 Komentara

    Safii sana Chelsea jembe langu kwa kujitahiji kubaki katika nafasi ya nne hivyo mnazidi kutupa mashabiki wenu nguvu mpya sasa kweli tangu mtoke katika kipindi kigumu cha corona mko vizuri sana

    Jibu

    Wanabahati sana ilikuwa bado kidogo tu watoke sare#Meridianbettz

    Jibu

    Chelsea wamepanda sana msimu huu mpak kufikia nafas ya nne iko poa sana na kuwaacha Manchester United kwa alama tano hivyo mechi ijayo akishinda atakuwa katika nafasi nzur sana
    Kwa upande wa Aston villa msimu huu wanaonekana hawako vzur sana
    Maana mchezo uliopita mpaka
    Kuwafanya watoke suluhu
    wanajikuta wapo katika wakati
    mgumu sana
    # meridianbet Tanzania

    Jibu

    Yalikuwa matokeo mazuri kwa chelsea kupata arama tatu na kujikita na kukaa katika nafasi ya nne wakifuatiwa na man u tafauti ya arama tano ipo safii kabisa ila mbaya kwa aston villa maana watashuka daraja kipigo hicho kinafanya kukaa kwenye nafasi mbaya zaid,champions ship inawahusu dah mtanzania mwenzetu bora angebaki gent ila sio mbaya labda atapata timu nyngine mchawi dua tu

    Jibu

    Matokea mazuri kwa Chelsea kupata arama ya tatu na kuwa katika nafasi ya nne mnazidi kuwapa moyo mashabikj wenu

    Jibu

    Pongez kwa Chelsea kuendelea kujikita nafasi ya nne ila waendeleze hvyo hvyo moto mpk mwisho wa msimu maana huyo alioko chini yake anaitaman hyo nafasi kwa hamu sana

    Jibu

    Kwl kwa upande fulan Chelsea imewavusha kuongezah gepu la point kwny mbio za top 4 ingawah Aston villa samata timu inazid kwenda chn Ila kwny foot ball hakuna huruma ndo mchezo wenye matokeo ya kikatil sana sema Aston villa nafas ipo iliwawez kupgana kutoshuka daraja na Chelsea nafasi wanayo kupambana top 4 thnks meridian bet tz kwa update za michezo

    Jibu

    Pongezi kubwa kwa chelsea ila msibweteke

    Jibu

    Aston villa Bax wajipange championship Tu

    Jibu

    Jahazi linaenda kuzama Aston Villa kiu ya watanzania kumtazama Samatta inapotea

    Jibu

    habari njema kwa mashabiki wa chelsea

    Jibu

    Villa walishindwa kiendeleza jihad yao kwenye hii mechi lakini uzoefu na umahiriwa chelsea uliwafanya waondoke na pointi 3

    Jibu

    Mi naamini kwenye ligi yeyote kila mmoja anaangalia nafasi yake

    Jibu

    ni kweli matoke mazr ya mchezo kati yake na astonivilla

    Jibu

    Maoni:hali sio nzuri kwa Aston villa

    Jibu

    Chelsea wako vizuri.

    Jibu

    Chelsea hongera sana ila muendelee kukaza msiwe wazembe

    Jibu

    Hongera wapo nafasi nzur katika msimamo wa ligi ila astonvilla wanapumulia mashine maskin samatta

    Jibu

    Katika mechi hii Chelsea walipindua meza kibabe sana hongera kwao

    Jibu

    Team samata ! mtu samehe kwa kweli sioni kabisa Kama Aston villa itabaki EPL

    Jibu

    hao ndo blue

    Jibu

    Maoni:Hongera sn chelsea mko vzur

    Jibu

    The blues endeleeni kunipa raha

    Jibu

    Aston Villa amekalia kuti kavu

    Jibu

    Chelseawako vizuri sana ila Aston villa wasikate tamaa kwa ilo wanatakiwa kujipanga kwa upya katoka msimu wa ligi

    Jibu

    Hongera sana Chelsea kujikita nafasi ya4 waendelee ivo ivo

    Jibu

    Pongezi ziende kwa Chelsea

    Jibu

    Pongezii kwa Chelsea 👏

    Jibu

    Pongezi kwao chelsea

    Jibu

    dah dua imekataa United bado hali mbaya

    Jibu

    Chelsea wako vizur wakaze buti ongera zao

    Jibu

    Chelsea imejitaidi waendelee kukaza butii wadiludi nyuma

    Jibu

    Astonvila njia ya kushuka daraja nyeupe

    Jibu

    Chelsea wako vizur kwa sasa

    Jibu

    Chelsea wako vizuri

    Jibu

    Hili lilikuwa wazi kwamba Chelsea lazima ashinde

    Jibu

    Heshima kwenu Chelsea

    Jibu

    Hongera sana Chelsea mmejitahidi Sana na mumeoneaha juhudi mpaka kufika nafasi ya nne

    Jibu

    Chelsea wanaweza kuchukua ubingwa

    Jibu

    Hongera kwao Chelsea mpira ulikuwa mzuri htr vikosi vilijiandaa vzr

    Jibu

    Chelsea wanaweza kuchukua ubingwa#meridianbettz

    Jibu

    Chelsea wamejipanga vizuri Sana

    Jibu

    Chelsea nyota bahati iko upandea wao

    Jibu

    mbaya kwa aston villa maana watashuka daraja kipigo hicho kinafanya kukaa kwenye nafasi mbaya zaid,champions ship inawahusu dah mtanzania mwenzetu bora angebaki genk Ila akuna kufeli#meridianbettz

    Jibu

    Aston Vila kazi hana

    Jibu

    Kweli hawajafanyia haki jamanii

    Jibu

    Vita iliyopo kwa timu zilizohatarini kushuka daraja kujiokoa na timu zinazotaka tiketi ya kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE#meridianbettz

    Jibu

    Namuona samatta akicheza championship

    Jibu

    Hongera Sana Chelsea kwa kubaki nafasi ya nne na hata pia Aston vila pia nao wasikate tamaa waendelee kukaza buti

    Jibu

    Duuuh kweli hawajamfayia haki

    Jibu

    Ze blues

    Jibu

    Sam Magoli amekwenda Uingereza kwenye wakati mbaya sana kwani itakuwa vigumu kumuona akilisakata soka kwenye ligi kuu ya uingereza hasa ukiangalia hali mbaya kwa Villa

    Jibu

    Gudaguda Chelsea kwa kuongeza point tatu tunatarajia mazur Zaid yajayo

    Jibu

    Chelsea ni timu nzuri na inawechezaji wazuri

    Jibu

    Chelsea wapo vizuri

    Jibu

    Chelsea wanafanya vizuri

    Jibu

    Jamani samatta wetu dahhhj

    Jibu

    Chelsea tuko vizurii

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.