Klabu ya Inter Milan wako tayari kufungua mazungumzo na klabu ya Manchester United kwaajili ya kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wao Alex Sanchez.
Alex Sanchez anaechezea kwa mkopo nchini Italia,ataendelea kuwepo katika klabu ya Inter Milan mpaka mwezi wa nane baada ya msimu wa mwaka 2019/20 kukamilika baada ya klabu hizo kukubaliana.
Sanchez alitakiwa kurudi katika klabu yake ya Manchester United mwezi wa sita tarehe 30, lakini hata ruhusiwa kucheza katika mashindano ya Europe League endapo Inter watafuzu.

Ataruhusiwa kucheza katika mchezo wa 16 bora dhidi ya Getafe mwezi 8 tarehe 5 au 6 ambao ulihairishwa kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu (Covid 19).
Kocha wa Inter Milan Antonio Conte amevutiwa na huduma za mchezaji huyo licha ya kuwa katika majeruhi kwa kipindi fulani,Kocha huyo alivutiwa zaidi hasa katika mchezo wao dhidi ya Brescia aliofunga na kutoa pasi mbili za magoli wakishinda goli 6-0.
Mchezaji huyo anathamani ya euro million 28, lakini raisi wa klabu hiyo Giuseppe Marotta ana uhakika wa kuweza kumsajili kwa punguzo la bei la euro millioni 20 katika kipindi hichi.


Samira
Mi natamani kumuona sanchez akimalizia soka lake pale pale man utd
Samiah
Good news👍
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri Kama yeye mahamuzi yake yapo sahii kuondoka haende tuu hakabadilishe hupepo
Dorophina
Ni bora Sanchez amalizie soka lake man u huko inter amna ht ishu
JULIANA
Waweke mkwanja mezani
Sadick
Inter inacheza kamari hatari sana. Sanchez kwaasa hawezi kurudia kiwango alichokuwa nacho akiwa Arsenal
Magdalena
Kama wanamtaka kikubwa ni dau tu la kutosha
isha
Wampe tuu dau nono ili aende akafanye yake
Johnmary joel
Hapo ni pesa ikipatikana wamchukue#meridianbett
Isaya massawe
Sijaona alichoifanyia man united pamoja na kulipwa hela nyingi tuu
Amani
Sanchez kwaasa hawezi kurudia kiwango alichokuwa nacho akiwa Arsenal
Neema juma
Pesa yao tu hakuna kitakachoshindikana
Genia Sikaluzwe
Pesa ndiyo musema kweli hakuna kinacho shindikana
Povel
Sanchez mwamba
Khadija
Sanchez kwa sasa hawezi kurudia kiwango alichokuwa nacho#meridianbettz
Rehema Dickson
Kama yeye mahamuzi yake yapo sahii kuondoka haende tuu hakabadilishe hupepo
Caroline
Alex Sanches ni mchezaji Mzuri sanaa
felister
Kama vipi arudi zake tu arsenal
Revina
Wasifanye masiala huyo mchezaji hata alipo bado wanamuitaji sema abadilishe upepo
Hamidu
Intermilan wamchukue tuu..kule man utd nafsi yake haipo kwa sasa#meridianbettz
Ernest
Safi sana Inter Millan kwa kuona kiwango na mchango wa Sanchez, jamaa anastahili kupata timu ya kucheza
Ester jackson
Sanchez kama akienda inter Milan si rahisi kabisa kurudi timu nyingine
Edgar
sunchez Kama nafanya vzr inter wacha tu wamchukue maana haliletwa kqa mkopo, hata lvyo pale man u alikua hayupo free kabisa Yan… Kanafanya vzr wamchukue tu.
nasra
Sanchez kiungo Bora
warda
Wamchukue Tu Wala Hatumtaki#Meridianbettz
Njiku
Man u Bora wa muuze tu sanchez maana Manchester hawamtumii mshambuliaji huyo bora wawauzi inter millan
Hope mwaikuka
Anafaa kwa matumiz kama wanamuhtaj wayajenge tu
Gabriel
Kiukwel Sanchez ameondoka kwenda Inter Milan kwa mkopo na kumuachia nafasi kubwa kinda wa miaka 17 Mason Greenwood chini ya Solskjaer. Meneja huyu ameweka wazi kuwa Smalling pia yuko mbioni kuelekea Italia kusainisha mkataba na klabu ya Roma na ukiangalia pindi alivyoondoka tunaona mpira wake umekuwa kwa kiwango kizur sana 👍
Issa
Sidhani kama united itakubali kumtoa sanchez jumla kwa inter sababu hawana uhakika wa pogba hivyo itakua ngumu kuwaachia
Angelina
Aende tu
fatumakasom
Kiungo mzur sana huyo
Furahav
Snchez yuko vizuri,wamchukue tu.
Saupha mohamed
Pesa mezani tuu
Rehema
Ni jembe Yuko fresh
Amiri Kayera
Ni mchezaj mzur inter imeona anamsaada mkubw ndomn awatak kumuachia
Devotha
Pesa ndo kila kitu! Waweke pesa wamsaini
Tahiya
Vizur kama watafikia makubaliano
Sabrina
Maoni:Bora wamuuze tu Man u wenyewe wanamuweka bench tu
Latifa juma mohamed
Day nono ndio mpango mzima
Latifa juma mohamed
Dau nono ndio mpango mzima
Salma
Vizuri kama watakubaliana
Theckla
Bado yuko vizuri Kama wakamchukua itakuwa imekaa vizuri
Omary lukumbi
Sanchez bora arud tuu man United maana kuna mafundi na timu iko njema kwa sasa hasa james bado ana utoto mwingi
Evaluziga
Wampe tu dau nono akafanye yake
David Pere
Ameonyesha kiwango kizuri Sana kwao Ndio maana wanamtaka mazima
Theonestina
Wapande dau tu
Tatu
Kama wakimchukua bado yupo vizuri
Shafii
Sanchez abaki hukohuko series A maaana hakua na wakati mzuri pale old trarfod.
lombo
saf