Ronaldo: Je, Lewandowski Atavunja Rekodi UEFA?

Mshambuliaji wa Bayern MunichenRobert Lewandowski amekuwa na msimu mzuri katika Bundesliga na Michuano ya Ulaya – UEFA msimu huu. Je, ataifikia rekodi ya Cristiano Ronaldo.

Lewandowski amechukua tuzo ya mfungaji bora kunako Bundesliga msimu huu na bado anawasha moto katika Michuano ya UEFA. Mpaka sasa, Lewandowski anajumla ya magoli 13 katika  mechi 7 za UEFA alizocheza msimu huu. Idadi hii ni pungufu kwa magoli manne ambapo Cristiano Ronaldo alifunga magoli 17 katika msimu wa 2013/14.

ronaldo
Orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa magoli Bundesliga

Endapo Bayern Munich watafanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya UEFA msimu huu, Lewandowski atakuwa na michezo mitatu mkononi ambayo anaweza kuitumia kuifikia rekodi ya Ronaldo.

Lewandowski akizungumzia jambo hili, amenukuliwa akisema ” Sio lengo langu. Bado tunamichezo kadhaa katika hatua ya mtoano na ninafurahia kutengeneza nafasi za magoli na kufunga pia”

ronaldo
Orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa magoli UEFA

Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi katika Michuano ya Ulaya – UEFA. Mpaka sasa, Ronaldo anamagoli 130 akimzidi Lewandowski kwa magoli 64. Ili Lewandowski afikie rekodi hiyo, anapaswa kufunga magoli 16 katika misimu minne ijayo na, hiyo itategemea kama Ronaldo atashindwa kuzifumania nyavu mda wote huo.

Lewandowski ameendelea kuonesha uwezo wake kama mshambuliaji hatari kunako anga za mpira wa miguu. Katika mchezo wa mtoano dhidi ya Chelsea, Lewandowski amehusika katika magoli 7 waliyoshinda Bayern Munich.

ronaldo
Lewandowski akishangilia goli dhidi ya Chelsea

Katika mchezo wa kwanza, Lewandowski alitoa pasi moja ya goli na kufunga goli moja. Katika mchezo wa pili, Lewandoski alitoa pasi 2 za magoli na kufunga magoli 2, hivyo kuhusika katika jumla ya magoli 6 katika mchezo huo akifunga magoli 3 na kutoa pasi 3.

Kwa msimu huu pekee, Lewandowski amefunga magoli 53 katika michezo 36 akiwa ameshacheza michezo 44. Kwa takwimu za misimu miwili iliyopita, ni Lionel Messi pekee aliyemzidi (95) Lewandowski (67) magoli na pasi za kufunga katika ligi zao.

ronaldo
Barcelona vs Bayern Munich

Bayern Munich watakutana na FC Barcelona katika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Ulaya – UEFA wikiendi hii.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma Zaidi

43 Komentara

    Dash kumfikia ronaldo kunataka nguvu zaidi na kupenda kucheka na nyavu sana hiyo ndio itamfanya amfikie ila atasukua gaga sana

    Jibu

    Kumfikia Ronaldo kunataka nguvu inatakiwa apambane zaidi afikie levo ya Ronaldo akijitaidi ataweza kwasababu yupo vizuri Lewandowski mpambanaji namtu mwenye uwezo wa kuitikisa nyavu

    Jibu

    Akijitahidi anaweza akafika lakini anatakiwa apambane mno bila hivyo ndoto zake zitaishia kwenye maji

    Jibu

    Lewandoski bado sana kwa Ronaldo.

    Jibu

    Niliamini Lewandowski angechukua Ballon D’Or msimu huu kama isingefutwa#meridianbettz

    Jibu

    Kama atambana atamfikia ronaldo ” hata mbuyu ulianza kama mchicha”

    Jibu

    kumfikia ronald itakuwa ngumu inatakiwa wapambane zaid#meridianbettz

    Jibu

    lolote linawezekana hakuna kinachoshindikana kikubwa bidii tu utakua kama yeye

    Jibu

    Maadam bado sio majeruhi inawezekana

    Jibu

    Tusubir tuone kama itawezekana

    Jibu

    Asante meridianbet kwa taarifa

    Jibu

    Kuwa Kama Ronald inabidi afanye mazoezi kwa wingi na asikate Tamaa iko siku atafanana naye@meridianbettz

    Jibu

    Kwa mechi zilizosalia anaweza akafikisha magoli 17 maana jamaa mpambanaji Sana.

    Jibu

    Lewandoski atachukua kiatu tu kwakuwa juve wametupwa nje

    Jibu

    Ni ngumu kufikia rekod ya magol maana hapa labda Ronald aumwe asicheze misimu yoyote maana Ronaldo anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi katika Michuano ya Ulaya UEFA Mpaka sasa, Ronaldo anamagoli 130 akimzidi Lewandowski kwa magoli 64. Ili Lewandowski afikie rekodi hiyo, anapaswa kufunga magoli 16 katika misimu minne ijayo na, hiyo itategemea kama Ronaldo atashindwa kuzifumania nyavu mda wote huo n Jambo ambalo sio kwel ila anauwezo wa kuchukua mchezaji bora isyohusu magol au labda itikee adhabu hivyo atafutwe mbadala wake wa kushindanishwa nahis itakuwa imekaa poa ila lewandowski n mchezaji mzur sana

    Jibu

    Axante kwa makala nzur

    Jibu

    Na amini hakuna lisilowezekana jitihada tu zinahitajika

    Jibu

    Bora tusubili tuone Kama itawezekana

    Jibu

    Bayern kama wataamua kumbeba Lewandowski basi ni kazi rahisi sana kwake kuvunja rekodi

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Lewandosk anatakiwa ajipange sana tu ili amfikie Ronaldo

    Jibu

    Kila kitu kinawezekana jini ya jua

    Jibu

    Lewondowski bado ana nafas ya kucheza anawez vunja rekod ya cr7

    Jibu

    Ahsant meridian kwa taarifa

    Jibu

    asante meridianbet kwa habar moto moto

    Jibu

    Thanks for update #meridianbettz

    Jibu

    Ngoja tujionee wenyewe

    Jibu

    Asanteni meridianbet kwa makala nzuri

    Jibu

    Ajipange sana

    Jibu

    Noma ngoja tuone

    Jibu

    Ni ngumu sanaa kivunja Record ya CR7 hakuna kabisaa

    Jibu

    Ni ngumu sana kumfikia mnyama cr7 hakuna mtu atakaye weza

    Jibu

    Kujiamini na juhud ndio mafanikio yake

    Jibu

    Anaweza labda kila kitu ni juhudi binafsi#Meridianbettz

    Jibu

    Bora tusubiri tuone kama itawezekana#Meridianbettz

    Jibu

    kijana mpaka kumfikia ronaldo anabidi afanye juhudi za kutosha sana ronaldo ni mtu mwingine kabisa katika mpira

    Jibu

    Kwa magoli ambayo robart lewandowsk amefunga 14 na mechi zilizobaki anaweza akaifikia record ya cr7 na akaivunja.

    Jibu

    Lolote linawezekana.Lewandowski yupo vizuri sanaaa

    Jibu

    Lewandowski yupo kwenye nafasi nzuri kuvunja rekodi ya CR7

    Jibu

    Ngumu sana

    Jibu

    Hii sasa ni wakat wa robert rewandosky maana ronaldo hayupo UEFA amebaki yeye na lionel mess tuu ila Robert yupo mbele kwa magoli zaid ya messi

    Jibu

    Asanteee kwataarifa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.