Mshambuliaji wa Bayern Munichen – Robert Lewandowski amekuwa na msimu mzuri katika Bundesliga na Michuano ya Ulaya – UEFA msimu huu. Je, ataifikia rekodi ya Cristiano Ronaldo.
Lewandowski amechukua tuzo ya mfungaji bora kunako Bundesliga msimu huu na bado anawasha moto katika Michuano ya UEFA. Mpaka sasa, Lewandowski anajumla ya magoli 13 katika mechi 7 za UEFA alizocheza msimu huu. Idadi hii ni pungufu kwa magoli manne ambapo Cristiano Ronaldo alifunga magoli 17 katika msimu wa 2013/14.

Endapo Bayern Munich watafanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya UEFA msimu huu, Lewandowski atakuwa na michezo mitatu mkononi ambayo anaweza kuitumia kuifikia rekodi ya Ronaldo.
Lewandowski akizungumzia jambo hili, amenukuliwa akisema ” Sio lengo langu. Bado tunamichezo kadhaa katika hatua ya mtoano na ninafurahia kutengeneza nafasi za magoli na kufunga pia”

Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi katika Michuano ya Ulaya – UEFA. Mpaka sasa, Ronaldo anamagoli 130 akimzidi Lewandowski kwa magoli 64. Ili Lewandowski afikie rekodi hiyo, anapaswa kufunga magoli 16 katika misimu minne ijayo na, hiyo itategemea kama Ronaldo atashindwa kuzifumania nyavu mda wote huo.
Lewandowski ameendelea kuonesha uwezo wake kama mshambuliaji hatari kunako anga za mpira wa miguu. Katika mchezo wa mtoano dhidi ya Chelsea, Lewandowski amehusika katika magoli 7 waliyoshinda Bayern Munich.

Katika mchezo wa kwanza, Lewandowski alitoa pasi moja ya goli na kufunga goli moja. Katika mchezo wa pili, Lewandoski alitoa pasi 2 za magoli na kufunga magoli 2, hivyo kuhusika katika jumla ya magoli 6 katika mchezo huo akifunga magoli 3 na kutoa pasi 3.
Kwa msimu huu pekee, Lewandowski amefunga magoli 53 katika michezo 36 akiwa ameshacheza michezo 44. Kwa takwimu za misimu miwili iliyopita, ni Lionel Messi pekee aliyemzidi (95) Lewandowski (67) magoli na pasi za kufunga katika ligi zao.

Bayern Munich watakutana na FC Barcelona katika hatua ya robo fainali ya Michuano ya Ulaya – UEFA wikiendi hii.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Ester jackson
Dash kumfikia ronaldo kunataka nguvu zaidi na kupenda kucheka na nyavu sana hiyo ndio itamfanya amfikie ila atasukua gaga sana
Lydia Emmanuel Magoti
Kumfikia Ronaldo kunataka nguvu inatakiwa apambane zaidi afikie levo ya Ronaldo akijitaidi ataweza kwasababu yupo vizuri Lewandowski mpambanaji namtu mwenye uwezo wa kuitikisa nyavu
aisha
Akijitahidi anaweza akafika lakini anatakiwa apambane mno bila hivyo ndoto zake zitaishia kwenye maji
Furahav
Lewandoski bado sana kwa Ronaldo.
Sadick
Niliamini Lewandowski angechukua Ballon D’Or msimu huu kama isingefutwa#meridianbettz
Salma ngende
Kama atambana atamfikia ronaldo ” hata mbuyu ulianza kama mchicha”
Khadija
kumfikia ronald itakuwa ngumu inatakiwa wapambane zaid#meridianbettz
felister
lolote linawezekana hakuna kinachoshindikana kikubwa bidii tu utakua kama yeye
Antony Luseno
Maadam bado sio majeruhi inawezekana
Tahiya
Tusubir tuone kama itawezekana
Rehema
Asante meridianbet kwa taarifa
Adelta
Kuwa Kama Ronald inabidi afanye mazoezi kwa wingi na asikate Tamaa iko siku atafanana naye@meridianbettz
Shafii
Kwa mechi zilizosalia anaweza akafikisha magoli 17 maana jamaa mpambanaji Sana.
Issa
Lewandoski atachukua kiatu tu kwakuwa juve wametupwa nje
Gabriel
Ni ngumu kufikia rekod ya magol maana hapa labda Ronald aumwe asicheze misimu yoyote maana Ronaldo anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi katika Michuano ya Ulaya UEFA Mpaka sasa, Ronaldo anamagoli 130 akimzidi Lewandowski kwa magoli 64. Ili Lewandowski afikie rekodi hiyo, anapaswa kufunga magoli 16 katika misimu minne ijayo na, hiyo itategemea kama Ronaldo atashindwa kuzifumania nyavu mda wote huo n Jambo ambalo sio kwel ila anauwezo wa kuchukua mchezaji bora isyohusu magol au labda itikee adhabu hivyo atafutwe mbadala wake wa kushindanishwa nahis itakuwa imekaa poa ila lewandowski n mchezaji mzur sana
Hope mwaikuka
Axante kwa makala nzur
Neema juma
Na amini hakuna lisilowezekana jitihada tu zinahitajika
Mwanahamisi
Bora tusubili tuone Kama itawezekana
Ernest
Bayern kama wataamua kumbeba Lewandowski basi ni kazi rahisi sana kwake kuvunja rekodi
Devotha
Asante kwa taarifa
Sabrina
Lewandosk anatakiwa ajipange sana tu ili amfikie Ronaldo
Tatu
Kila kitu kinawezekana jini ya jua
Povel
Lewondowski bado ana nafas ya kucheza anawez vunja rekod ya cr7
Genia Sikaluzwe
Ahsant meridian kwa taarifa
lombo
asante meridianbet kwa habar moto moto
MnonganeJR
Thanks for update #meridianbettz
farida ahmadi
Ngoja tujionee wenyewe
Theonestina
Asanteni meridianbet kwa makala nzuri
Saupha mohamed
Ajipange sana
Fatuma kasomo
Noma ngoja tuone
David Pere
Ni ngumu sanaa kivunja Record ya CR7 hakuna kabisaa
Dorophina
Ni ngumu sana kumfikia mnyama cr7 hakuna mtu atakaye weza
Rose kapinga
Kujiamini na juhud ndio mafanikio yake
warda
Anaweza labda kila kitu ni juhudi binafsi#Meridianbettz
Mwajumah
Bora tusubiri tuone kama itawezekana#Meridianbettz
magdalena
kijana mpaka kumfikia ronaldo anabidi afanye juhudi za kutosha sana ronaldo ni mtu mwingine kabisa katika mpira
Zeiyana
Kwa magoli ambayo robart lewandowsk amefunga 14 na mechi zilizobaki anaweza akaifikia record ya cr7 na akaivunja.
Caroline
Lolote linawezekana.Lewandowski yupo vizuri sanaaa
Nasra
Lewandowski yupo kwenye nafasi nzuri kuvunja rekodi ya CR7
Leonard
Ngumu sana
Omary lukumbi
Hii sasa ni wakat wa robert rewandosky maana ronaldo hayupo UEFA amebaki yeye na lionel mess tuu ila Robert yupo mbele kwa magoli zaid ya messi
Fatina mfingi
Makal nzur
Samiah
Asanteee kwataarifa