Leipzig wanaondoka, ila sidhani kama mioyo yao imeinama kwa masononeko. Wanafika nusu fainali ya UEFA miaka 11 tu baada ya kuanzishwa. Tena wanatoka wakiwa wamepambana katika ubora wa hali ya juu. Timu zingine zimetumia nusu karne kupata nafasi ya kushiriki.
Katika siku ambayo Neymar aliikumbuka miguu yake aliyoiacha Barcelona, katika siku ambayo Mbappe alikuwa katika ubora wa hali ya juu, siku hiyohiyo Di Maria akaupata ubora aliokuwa nao Lisbon katika fainali ya UEFA, ungehitaji muujiza kuwazuia PSG wasikufunge chini ya mabao matatu. Kwangu mimi, mechi iliamuliwa na ubora wa wachezaji zaidi ya mbinu za waalimu.
Leipzig walifanya makosa mengi kwenye eneo lao la ulinzi. Pasi zao ziliishia miguuni kwa viungo au washambuliaji wa PSG mara kadhaa. Hii ilitokana na namna PSG walivokaba pindi tu walivopoteza mpira. Bahati njema kwao PSG hawakuwaadhibu kwa kila kosa walilofanya.
Julian Neglesman, aliufahamu ubora wa washambuliaji wa PSG. Akawataka wachezaji wake wawasubiri PSG katika eneo lao badala ya kuwafanyia ‘pressing’ katika kipindi cha kwanza. Sikushangaa kuona Nafasi walizozitengeneza PSG zilitokana na mipira mirefu licha ya kuwa na umiliki mkubwa wa mpira.
Plan yake ilikuwa sahihi sana, makosa tu ni hawakujua namna ya kuondoka pindi walipoupata mpira. Mabao mawili ya PSG yametokana na mabeki wa Leipzig kushindwa kuondoa hatari, wakitaka kucheza pasi na viungo wao.
Anaimbwa Neymar, anaimbwa Mbappe, lakini yupo mtu nyuma ya majina yao. Huyo mtu ni Angel Di Maria. Mikimbio yake na maamuzi yake, yanawarahisishia kazi akina Neymar. Assist na bao akiwa katika kiwango bora, kwa jana yeye ndiye man match.
Hakuna mtu aliyefurahia kuitazama hii mechi kama kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps. Wakati akiliwaza fumbo gumu analopewa na Raphael Varane ghafla anakutana na jawabu rahisi kutoka kwa Kimpembe. Wakati anateswa na mtihani mgumu wa kiwango kibovu cha Samuel Umtiti, ghafla analetewa majibu na kijana mdogo Dayot Upamecano. Huo ukuta wa Ufaransa. Watu watakoma!
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Devotha
Ilikua mechi nzuri Sana upande wa PSG Ila nawapongeza pia RB Lepzig kwa hatua waliyoifikia kwao ni furaha
Shafii
Rb Leipzig wanastahili pongezi kwa kiwango walicho kionyesha kwenye mashindano hayo cha msingi wajipange tena kwa msimu ujao kwani mshindi wamashindano ni mmoja tu.
Povel
Di MARIA anastail pongez kubwa sana na kocha wa Rb liepzng anastail pongez kocha kijana kuifikisha mbal timu yake na vle vle na yy mafanikio yake binafsi
Theckla
Dimaria anahtaj pongezi xana
Adelta
Hongera kwake
@meridianbettz
Mwajumah
Ilikua mechi nzuri sana kwa upande wa psg pia dimaria anahitaji pongez sana#Meridianbettz
Sauda
Dimaria anastahili pongezi.
Dorophina
Leipzing walijitahidi sana kufanya vizuri ingawa walishindwa inabidi wajipange msimu ujao
Ernest
Mara nyingi PSG Wamekuwa watu wa kucheza mpira mwingi mechi na mechi, Ni kweli walikuwa katika high peak kwenye nusu fainali lakini wasiwasi wangu wanaweza wasituonyeshe kiwango hichi kwenye fainali
Fatina mfingi
Makala saf
Zeiyana
Leipzig wanaweza kumuita mbappe mchawi wao ukiangalia sana pale clabuni PSG mbappe amekua na moto mbio zake zote kuipelekea clabu yake kucheza fainali ya mabingwa
Khadija
dimaria anashili pongezi
Ester jackson
Safu iliyo kamilika kabisa PSG ukiangalia utatu ulio bora zaidi lazima uwataje vijana matata sana dimaria ,mbappe na neyrmaa hapo hautachoka kuangalia mchezo nasubiri kuona itakuwaje wakikutana na wazee Wa kukandamiza Bayern Munich
aisha
Psg wako vizuri sana wanasitahili pongezi
Mwanahamisi
Hongera kwake
Magdalena
di maria ni mahili sana katika soka namkubali sana
Lydia Emmanuel Magoti
Di Maria namuerewa Sana kwenye soka yupo vizuri
Johnmary joel
Kwakweli wmejitahidi sana#meridianbett
Saupha mohamed
Anastahili pongezi
Furahav
Anajua sana.
Gabriel
Yuko vzur sana di Maria
Amiri Kayera
Mafanikio yake yanatokan na team
Sabrina
Di maria yupo vizuri sana
Janeflora malisa
Nice
Theonestina
Hongera kwake
David Pere
Leipzig walifanya makosa mengi kwenye eneo lao la ulinzi. Pasi zao ziliishia miguuni kwa viungo au washambuliaji wa PSG mara kadhaa. Hii ilitokana na namna PSG walivokaba pindi tu walivopoteza mpira. Bahati njema kwao PSG hawakuwaadhibu kwa kila kosa walilofanya.
warda
Mna Habari nzuri sana
felister
mafanikio yake yanatokana na timu
Hope mwaikuka
Mtu mbad