Tetesi zinasema Baba yake Lionel Messi ameiambia Paris St-Germain kwamba mshambuliaji huyo wa Barcelona na Argentina, 33, anataka kujiunga na Manchester City.
Messi alimpigia simu kocha wa Manchester City Pep Guardiola Jumanne iliyopita, kabla ya kuiarifu Barcelona kwamba anataka kuondoka klabu hiyo na kumwambia kuwa ”Nataka kushinda tuzo mbili za Ballon d’Or, na naweza tu kufanikiwa kutimiza hilo nikiwa na wewe”.

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amekataa kukutana na Messi kujadiliana kima chake na anashikilia kifungu cha kuwezesha uhamisho wake cha pauni milioni 624.
Chelsea imeonesha nia ya kutaka kumsajili mlinda lando wa Italia Gianluigi Donnarumma, 21, ambaye anasemekana thamani yake ni pauni milioni 50 lakini ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na AC Milan.
Hatahivyo, AC Milan inafanya mazungumzo ya kumsajili tena mlinda lango wa Bournemouth Asmir Begovic baada ya kuwa na mchezaji huyo wa Bosnia, 33, kwa mkopo kuziba pengo la Donnarumma kwa kipindi cha nusu ya pili ya msimu uliopita.
Wakati huohuo, Chelsea huenda pia ikaongeza pesa zake za matumizi za msimu hadi zaidi ya pauni milioni 250 baada ya kufikiria kutoa ofa ya pauni milioni 80m kwa kiungo wa kati wa West Ham na England, Declan Rice, 21.

Jurgen Klopp aondoa uwezekano wa Lionel Messi kuelekea Liverpool lakini kocha wa Reds akubali kwamba raia huyo wa Argentina atakuwa na umuhimu mkubwa kwenye Ligi ya Epl.
Inter Milan iko katika hatua ya mwisho ya majadiliano ya pauni milioni 1.34 kumsajili beki wa kushoto wa Roma kutoka Serbia Aleksandar Kolarov, 34.
Tetesi zinasema Freiburg na mlinzi wa Ujerumani Robin Koch, 22, amefikia makubaliano binafsi na Leeds United.
Tetesi zinasema Kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 29, anawindwa na Barcelona.
Beki wa kulia wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 28, atafanyiwa vipimo vya matibabu na Tottenham Jumamosi baada ya kukubali kulipa kima cha awali cha pauni milioni 12 kwa Wolves. (Football London)
Mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 28, yuko huru kuondoka Liverpool na kujiunga tena na aliyekuwa kocha wa Southampton Ronald Koeman Barcelona.

Aston Villa iko tayari kumaliza ushindani na Sheffield United na Fulham kwa kufikia makubaliano ya pauni milioni 12 ya beki wa kulia wa Nottingham Forest Matty Cash, 23.
Real Betis inamnyatia mlinda lango wa Chile Claudio Bravo, 37, ambaye sasa yuko huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Manchester City mwisho wa msimu.
Kiungo wa kati wa Uhispania wa Under-21 Brahim Diaz, 21, anakaribia kujiunga na AC Milan kutoka Real Madrid.
Mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 29 aliamua kuikacha Barcelona kabla ya kushawishiwa kubaki na Meneja mpya wa timu hiyo Ronald Koeman.
Mshambuliaji wa zamani wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, amekubali mkataba mpya wa mwaka mmoja kusalia AC Milan, mkataba unaoaminika kuwa na thamani ya £6m.

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo, 35, amezima tetesi kuhusu mustakbali wake kwa kusema kwamba anajiandaa kwa msimu wa tatu Juventus.
Kuwasili kwa beki wa kulia raia wa Ireland, 28 Matt Doherty katika timu ya Tottenham kutoka Wolves kunaweza kuwa tiketi ya mlinzi wa Ivory Coast, Serge Aurier, 27, kuondoka.
Tetesi zinasema Tottenham imekataa ofa ya kwanza kutoka AC Milan kwa ajili ya Serge Aurier, huku Bayer Leverkusen ikionyesha nia ya kutaka huduma ya mlinzi huyo.
Tetesi zinasema Manchester United imewasilisha ombi la kumnasa kiungo wa Brescia Sandro Tonali, 20, ambaye anatajwa kama mmoja wa makinda wanaokuja juu nchini Italia.
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


rama
barcelona wamuachie tu messi aondoke akapate changa moto nyingine
Ester jackson
Naona messi sasa anataka kuwa Manchester city pamoja na kocha Pep Guardiola kurudisha ndoto zake Mimi kama shabiki nasubiri tu kuona anakuwa wapi
Dorophina
Kama kweli ni vizuri Messi kwenda man City akarudi kwenye chama lake la zamani wakashilikiane vizuri na guardiola
Devotha
Asante kwa taarifa
Mwajumah
Asante kwa makala
felister
Messi amekaa sana apo barca ni Bora sasa aende kwenye vilabu vyengine apate changamoto
Tatu
Kuna uwezekano wa mess kuamia man city
Fatina mfingi
Messi badili upepo na ww!
Caroline
Asante meridianbet Kwa taarifa
Ernest
Nazidi kufurahishwa na Leeds United jinsi wanavyofanya usajili ili kujipanga kwenye ushindani zaidi
Povel
Nice information
Fatuma kasomo
Aende kokote kila heri
Mwanahamisi
Asante kwa makala
Lydia Emmanuel Magoti
Akuna kingine Apo Messi ndio msema kweli Messi ndio mwenye uwamuzi wakuongea chochote kile yeye sehemu atakapo kwenda
Latifa juma mohamed
Maamuz ni yake mwenyew.
Agness
Nihabari njema
Nasra
Asantee kwa makala
aisha
Muacheni aamue yeye mwenyewe maana kila siku naona kama anazungumziwa
Amiri Kayera
Haya magazet let’s see sehem gan mess ataend
Rehema
Shukurani kwa makala
farida ahmadi
Messi maamuzi yake binafsi kuondoka hama kubaki Barcelona
Rose kapinga
Messi gumzo mjini!!
Sabrina
Akitua man city itakua Poa sana
Hope mwaikuka
Ni mda mrefu kaitumikia barca kama akiona ni sahihi kutoka sawa as long as yy atakua poa
Furahav
Habari nzuri.
Amani
Kwa Messi naona mahali sahihi pakwenda Ni man United
Samiah
Nice
lombo
saf
Saupha mohamed
Safi
Zeiyana
Messi kwa hatua hanayo haliyo fikia inaonesha zaili kabic hanampango na barcelona tena na ndio inavyo kuaga wachezaji mastar wanachagua wenyew kuichezea timu wanazo zipenda
Asia Abdy
Wacha tuone
Issa
Usajili ww mess utasumbua
Janeflora malisa
Good
Sauda
Messi hawezi kuondoka Barcelona
warda
Mie nasubilia tu ligi ianze
Johnmary joel
Haya sasa tunasubili kuona messi Anelka wapi#meridianbett
magdalena
messi bora tu aende city
aisha
Mess kuikacha fcb atavunja rekodi ya dunia kwa usajili
Khadija
tinasubil lig hianze
Shafii
Dirisha likishafungwa tutajua nani kaenda wapi nani kabaki.
David Pere
Naona messi sasa anataka kuwa Manchester city pamoja na kocha Pep Guardiola kurudisha ndoto zake Mimi kama shabiki nasubiri tu kuona anakuwa wapi
Gabriel
Makala imekaa poa sana 👍