Swali la kwanza la kujiuliza kwa Van de Beek ni anaenda kucheza nafasi gani? Jibu la swali la kwanza linaweza kuwa mwanzo wa swali la pili. Anakwenda kuchukua nafasi ya nani? Unakapokosa jibu la swali la pili, ndipo linapoibuka swali la tatu, kwanini Man United wamemsajili?
Msimu uliopita ameifungia Ajax mabao 13, akizidiwa na Hakimi Ziyech pekee. Alikuwa na wastani wa touches 7.8 kwenye box la wapinzani, ni zaidi ya mchezaji yoyote wa Man United kwa msimu uliopita. Zaidi ya yote, ni Bruno peke yake alifanikiwa kufunga, kupiga mashuti na kutoa assist zaidi yake. Ukitazama namba kama hizi, unawaza kwanini asianze katika kikosi cha United?
Unapojaribu kujijibu, linakuja swali, nani ampishe ili apate nafasi? Pogba na Bruno walitengeneza ‘muunganiko’ imara sana mwisho msimu uliopita. Ole Gunner Solksjaer hawezi kuwa kichaa kuwatenganisha tena.

Muhanga mkubwa anaweza kuwa Nemanja Matic. Donny ana wastani wa kupora mipira mingi zaidi ya viungo wote wa United. Isitoshe amewahi kucheza kama kiungo mkabaji, huenda Solksjaer anafikiria kumchezesha kama kiungo mkabaji, ili kumrahisishia majukumu Paul Pogba ya kuchezesha timu.
Pengine Ole anawaza kumtumia Doony kama mbadala wa viungo wake watatu. Ole anajua huwezi kubeba ubingwa bila kuwa na benchi imara. Liverpool walitwaa taji wakiwa na Keita na Milner nje, Guardiola alilitwaa akiwa na Mahrez nje. Ole hajasahau mateso aliyoyapata bila Pogba msimu uliopita. Anajua maana ya kikosi kipana.
Hata kama atapata nafasi katika kikosi cha kwanza, Van de Beek bado ana kazi ya kufanya. Viungo wachezeshaji wa Ajax hawajawahi kuwa na maisha mepesi ndani ya epl. Nishikie bia yangu wakati namkumbuka Davy Klaasen, nisogezee glasi wakati naitafuta picha ya Siem De Jong, kaa tuyajenge wakati naukumbuka mwanzo wa Christian Eriksen.
Donny anakuja akiwa bora ila ana kazi ya kupata nafasi katika kikosi cha United. Unahitaji muujiza kumpoteza Pogba au Bruno. Unahitaji moyo wa chuma kuchaguliwa mbele ya Matic. Bado tusisahau alipoishia Fred. Bado tusisahau alipoanzia Mctominay. Donny kazi anayo!
SHINDA NA HI LO
Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.


magdalena
endapo juhudi zake na jitihada zikwa nzuri anaweza akapewa nafasi ya kucheza
Mwajumah
Asante kwa makala#meridianbettz
Ester jackson
Hapo ndio utakuwa balaa sana man u mana namba anazo cheza zina wababe wanzuri anakazi ya zuada kuwafanya wachezaji aliowakuta wampigie saluti ili kupata nafasi zaidi ya kucheza uwanjani
Fatina mfigi
Hapo inatakiwa juhudi na jitihada tyu mbona nafasi hatapata!!
Sauda
Apambane ili kufikia malengo.
Caroline
Tumkaribishe Kwanza mengine baadae yatajulikana.karibu Sana Van de Beek
Tatu
Van de beek anaweza kuchezeshwa kwa number yoyote na akafanya vizuri
Ernest
Hapa ndo wachezaji wengi huanza kujuta kwanini nimekubali kuja huku zaidi unakuwa hupati muda mwingi wa kucheza na kuishia bench tuu kwa muda mrefu
felister
mpk wamesajili mimi nadhani nafasi yake ipo ndo mana akasajiliwa
Mwanahamisi
Apambane ili afikie malengo yake
Adelta
Ajipange na aonyeshe juhudi atapata nafasi ya kucheza@meridianbettz
Dorophina
Kila lakheri van de breek
[email protected]
Apambane ili afike malengo yake
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri akaribie Man U Sasa Apo picha linaanza namba zote Zina wenyewe alafu wababe wa kulisaka kabumbu Sasa Kaz ipo akikaza but anaweza akapata namba
Sadick
Kwa uchambuzi huu ina maana timu zinasajiri wachezaji ktk nafasi ambazo hakuna upungufu mkubwa#meridianbettz
Shafii
Cha msingi yeye inapaswa ajitume kwa dhati anapokua amepewa nafasi ya kucheza.
Nasra
Kutoa kwake ndio kutamsaidia
Genia Sikaluzwe
Kila la kheri van de breek
Issa
Van lete utam wa kiholanz united msimu huu watakaa tu
JULIANA
Asante kwataharifa
Khadija
Kila la kheri#meridianbettz
Rose kapinga
Sasa wamemsajili wa nn wakati hata namba ya kumpa hawajui?
Hope mwaikuka
All ze best to him
Saupha mohamed
Jamaa anajua ndomaana kasajiliwa
Frank
Pogba akiwa free plus bruno tutaona kitu kipya next season
Elika
Hapo ni kupambana mwanzo mwisho
Juliet
Uyu jamaa noma anajua sanaa
Shani
De beek ni kiungo ataeleta upinzan safu ya kiungo unitd
Neema
Naaminii hatowaangushaa huko aendako
Samiah
Asanteee kwa taarifa
Sabrina
Ajitahidi tu
Agness
Asante kwa makala meridian
Rehema
Asante kwa makala
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Povel
Big Deal
Amiri Kayera
Usajir mzur
Gabriel
Kila lakheri van de breek
warda
Atapata tu nafasi