Juventus: "Alvaro Morata Amerejea Jijini"

Juventus wamempa ukaribisho nyota Alvaro Morata ambaye anatarajia kurejea Turin kwa mabingwa hawa wa Serie A.

Morata anatajwa kuwa anajiandaa kurejea Juventus kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Atletico Madrid kwa dili lenye thamani ya Euro milioni 9 huku Juve wakiwa na chaguo la kumnunua kwa Euro milioni 45.

Kufika kwa Morata, Juventus wanaweza kupumua baada ya jitihada zao za sokoni za kuongeza Fowadi kikosini kwao.

Kupitia ukurasa wao wa Twitter, Juventus walichapisha kuwa “Morata amerejea mjini” wakiambatanisha na picha za fowadi huyo.

alvaro morata-atletico
Alvaro Morata anatarajia kuichezea Juvetus kwa mwaka mmoja.

Morata tayari alishakuwepo Juventus, ambapo alicheza mechi 93 na kufunga magoli 27 kwa misimu kati ya 2014 na 2016.

Kisha alirejea Real Madrid kwa msimu mmoja kabla ya kuungana na Chelsea kisha Atletico Madrid. Msimu uliopita alifunga magoli 12 katika mechi 34 za LaLiga.

Alvaro Morata anarejea Juventus wakiwa wanahusishwa na Luis Suarez wa Barcelona na Edin Dzeko wa Roma, baada ya kuondoka Gonzalo Higuain kwenda Inter Miami.

Chapisho la mwisho la Juventus kwenye ukurasa wao wa Twitter ni kumtakia heri Morata katika vipimo vyake.

Juve wanatarajia kuendelea na utawala wa Serie A, wakilitafuta taji lao la 9 mfululizo baada ya kuanza vyema mechi ya ufunguzi kwa kuwachapa Sampodoria 3-0.


 

FURAHIA KASINO YA MTANDAONI

Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.

Cheza Sasa

.

36 Komentara

    Alvaro karibu Juventus.usituangusheee

    Jibu

    Yupo sehemu sahii morata juve wamepata mchezaji hanaye jituma

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    nina imani ukikutana na ronaldo utajifunza mbinu tofauti nzuri sana karibu juve kijana

    Jibu

    Alvaro kabibu kwenye chama ukipige vizuri

    Jibu

    Kila lakheri alvaro

    Jibu

    Alvaro Morata anaelekea ukingoni mwa soka lake mara Chelsea, mara Atletico na sasa amerejea Juventusna endapo hatafanya vzr atapotea jumlajumla#meridianbettz

    Jibu

    Sio sababu ya morata kuondoka ateltico bora angebaki kule

    Jibu

    Kikubwa asituangushe huko aendako

    Jibu

    Apige kazi

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Alvaro Morata anarejea Juventus wakiwa wanahusishwa na Luis Suarez wa Barcelona na Edin Dzeko wa Roma, baada ya kuondoka Gonzalo Higuain kwenda Inter Miami imekaa poa sana 👍

    Jibu

    Alvaro karibu sana Juventus utuoneshe kipaji chako

    Jibu

    Alvaro karibu Juventus

    Jibu

    Vizur

    Jibu

    Good

    Jibu

    Heshima ya Álvaro Borja Morata Martín imeshuka sana sio yule Morata ambaye tunamfahamu alafu cha Ajabu bado umri haujamtupa mkono kivile

    Jibu

    Morata anaenda kufanya maajahu juve

    Jibu

    vizuri sana

    Jibu

    Pambana Alvaro tuko nyuma yako

    Jibu

    Tunasubiria tuone ataenda kufanya maajabu yapi

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Morata amepotea sana sijui kiwango chake kimeshuka mana tangu atoke Chelsea simsikii tena kuwa mahiri na mpira

    Jibu

    Morata anajua anachofanya kwenye pitch

    Jibu

    saf

    Jibu

    Morata anajitambua na pia anafaham anachokifanya

    Jibu

    Morata inabid aongez kiwango

    Jibu

    Good

    Jibu

    Alvaro karobu jijini

    Jibu

    Mimi nina imani utafanya vizuri

    Jibu

    Apige kazi

    Jibu

    Kila la kheri kwake

    Jibu

    Pongezi kwa wakala wake maana anajua kumsimamia aisee

    Jibu

    Vizuri sana

    Jibu

    nina imani ukikutana na ronaldo utajifunza mbinu tofauti nzuri sana karibu juve kijana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.