Simeone: Joao Felix Ataendelea na Kasi Aliyoanza nayo.

Joao Felix ameuanza msimu mpya vyema kabisa na kocha Diego Simeone anatumaini mshambuliaji huyo wa Atletico ataendelea na kiwango hicho awamu hii.

Baada ya kutua akitokea klabu ya Benfica kwa dau la €126m, Joao Felix amehusika kwenye magoli mawili na asisti moja katika michezo sita aliyocheza msimu 2019-20 lakini anakumbukumbu yakupata majeraha mara kwa mara kitu kilichopelekea kutokuwa katika kiwango kizuri.

Atletico tayari wameuanza msimu mpya kwa kuikung’uta 6-1 timuya Granada katika mchezo huo Joao Felix alifunga goli lake la kwanza msimu huu kwa mkwaju wa penati pia alitoa asisti kwa Angel Correa.

Simeone: Joao Felix Ataendelea na Kasi Aliyoanza nayo.
Joao Felix

Ingawa mchezo uliyofuata Atletico ililazimishwa sare ya kutofungana na timu iliyopanda daraja Huesca katikati ya wiki Joao alijaribu kupiga mashuti sita kwenye lango la Huesca na kutengeneza nafasi mbili kwa mchezaji mwenzake.

Diego Simeone ambaye ni bosi wa Atletico anatarajia kuona mengi kama hayo kutoka kwa mreno huyo na Timu yake itakutana na Villarreal katika dimba la Wanda Metropolitano siku ya Jumamosi.

“Msimu uliyopita kwenye pre-season alikuwa na kiwango kizuri ni sawa na hiki anachokionesha sasa,” Simeone alisema na waandishi wa habari siku ya Ijumaa.

“Katika michezo minne mitano alikuwa imara mpaka pale alipopata majeraha, alikuwa na mwanzo mzuri msimu ule.

Atletico ilipoteza michezo minne pekee katika LaLiga msimu ulliyopita na kutoa sare 16 na kumaliza nafasi ya tatu wakiwa nyuma ya mabingwa Real Madrid kwa alama 17.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

31 Komentara

    Aongeze mwendo, asirudi nyuma

    Jibu

    kijana anaendelea kupamba moto kila kukicha

    Jibu

    Akaze buti

    Jibu

    Akaze mwendo

    Jibu

    Joao Felix ni mchezaji mzuri sana kama ataendela kuwa katika ubora huu basi tutarajie kusikia mengi juu yake miaka ijayo

    Jibu

    Joao ni mchezaji mzuri sana amekuja vizuri na anaspeed akiendelea ivyo atafika mbali

    Jibu

    Vizuri Sana Simeone kaza buti utafika tuu jembe

    Jibu

    Felix Ni mchezaji mzuri sana

    Jibu

    Ferix ni mchezaji mzur binafsi mimi namuelewa sana

    Jibu

    Akaze buti tu

    Jibu

    Diego simeone ategemee kushuhudia mazuri kutoka kwa mchezaji joao felix ambae alisajili kwa dau nono

    Jibu

    Diego yupo sahii kama atletico watamtumia vizuri Felix hatabadirisha matokea kwenye clabu hiyo maana amekua na moto wajabu

    Jibu

    Felix anafanyaga mabadiliko mara nyingi

    Jibu

    Joao felix usituangushe tunakuaminiaa

    Jibu

    akaze buti

    Jibu

    Safi sana inapendeza kijana

    Jibu

    Itapendeza sana

    Jibu

    Akaze buti

    Jibu

    Simeone ana kikosi kizur sana felix ni moja ya wachezaj tumain kwa simeon

    Jibu

    Felix yuko vizuri sana

    Jibu

    Felix joa ngoj tuone

    Jibu

    Amekua kweny kiwango kizur

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Akaze kamba Zaidi.

    Jibu

    Akazee

    Jibu

    Felix ni mchezaji mzuri sana kama ataendela kuwa katika ubora

    Jibu

    Nyota njema hiyooo

    Jibu

    Itakua poa sana akiendelea vizuri zaidi

    Jibu

    Joao Felix ni mchezaji mzuri sana kama ataendela kuwa katika ubora huu basi tutarajie kusikia mengi juu yake miaka ijayo

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.