Kama ni mdau wa soka na umefatilia dirisha la usajili lililomalizika mapema Jumatatu, utakumbuka mkasa wa Luis Suarez kutoa chozi wakati akiongea na waandishi wa habari.
Tukio lile liliteka vichwa vya habari duniani kutokana na uwezo mkubwa wa mshambuliaji huyo. Lakini ni nini hasa kilimfanya Suarez kumwaga machozi alipokuwa akiwaaga mashabiki wa Barcelona mbele ya waandishi wa habari?
Suarez anasema sababu kubwa ni namna alivyokuwa akiishi ndani ya klabu hiyo, baada ya kuitumikia Barca kwa miaka 6, mshambuliaji huyo ilifikia hatua akasimamishwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza kabla hajaondoka kwenye timu hiyo, inasikitisha!

” Zilikuwa ni siku ngumu sana kwangu, nililia kwasababu ya niliyokuwa ninayapitia. Niliumizwa sana kwa namna mambo yalivyokuwa yanafanywa, kwasababu tu mtu anapaswa kukubaliana na hali pale anapokuwa amemaliza muda wake.
“Sikukubalina na ujumbe wa klabu kwamba wanatafuta suluhisho la hali yangu kwasababu kiuhalisia haikuwa hivyo.
“Sio kila mtu anajua kilichokuwa kinafanyika, lakini kitu kibaya zaidi ni kwenda mazoezi halafu unapelekwa kwenye kundi lingine kwasababu hauruhusiwi kufanya mazoezi na wachezaji wengine.
“Mke wangu alishuhudia ni kwa jinsi gani sikuwa na furaha, alihitaji kuniona nikitabasamu tena na ilipotokea fursa ya kujiunga na Atletico Madrid, sikuwa na mashaka yoyote.
“Sikushangaa kumuona Messi akiwanisapoti mbele za watu, ninafahamu vizuri. Anajua maumivu niliyokuwa ninayapitia, hisia za kufukuzwa ziliniumiza sana.
“Namna wanavyofanya kazi haikuwa sahihi na Leo [Messi] anajua ni kwa namna gani mimi na familia yangu tulivyotaabika.”
Suarez alijiunga na Barca 2014 akitokea Liverpool kwa dau la pauni milioni 74, amefunga magoli 198 na amebeba mataji kadhaa ikiwemo LaLiga, Capa Del Rey na UEFA Champions League.
Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!


Issa
Suarez streika hatari kwnye 18 na majeraha tu ndio yanamrudisha nyuma
Angelina
Yuko vizur suarez
Hopemwaikuka
Kumbe ilkua hvyo
Povel
Hapo ndipo nakumbuk msemo wa waswahil TENDA WEMA NENDA ZAKO usitegemeeh walimwengu watakulipah fadhila hapa dunia ndo kinachotokea kwa mwamba suarez magoli ndani ya nou camp sasa
David Pere
Hapo ndipo nakumbuk msemo wa waswahil Tenda wema wende zakooo usitegemeeh walimwengu watakulipah fadhila hapa dunia ndo kinachotokea kwa mwamba suarez magoli ndani ya nou camp sasa
Mwanahamisi
Yuko vizuri suarez
magdalena
suarez ametoka katika timu amabayo alikuwa anapewa ushirikiano mzuri na wachezaji wenzie ila uko alikoenda na imani atakuwa bora zaidi
Adelta
Suarez Yuko vizuri na anajuwa vyema anachokifanya
Ernest
Legend ataendelea kuwa Legend tuu
Caroline
Pole Sana Suarez
Lydia Emmanuel Magoti
Duu pole Sana Suarez
Venerose
Mmmh
Zeiyana
Pole sana Suarez na hayo ndio maisha ya mpila na siku zote mtu hawezi kuona humuhimu wako ukiwa karibu nae unaweza ukasema kocha hana makosa hau uwongozi akuna yote kwa yote kupelekea kutaka timu hiwe kwenye ubora ila sizani kama Barcelona watasahau kazi yako uliyoifanya kwenye clabu ile history yako haiwezi kufutika
Tatu
Nora tu ulivyosepa Suarez maana uwezi kufanya jambo bila kuwa na furaha moyoni mwako kila la khery huko uwendako ila Barcelona watakukumbuka kwa mchango wako na mapenzi ya dhati huko kwenye timu yao
Janeflora malisa
Kumbe
Sadick
Duh! watu wamesahau mchango wake wa kihistoria wa kufunga magoli 198#meridianbettz
Rehema
Duuuh
Sabrina
Duuh pole sana suarez
aisha
Yuko vizuri sana lakini majeraha ndio mtihani kwake
felister
pole suarez
Fatuma kasomo
Gud news
Nasra
Pole suarez
Amiri Kayera
Hakupew eshima anayostyle
Shani
Barca imemfanyia sio suarez mchezaji alijitoa kwa barca
latifa juma mohamed
Yuko vizur suarez
Saupha mohamed
Duuh
Sauda
Pole yake
Gabriel
siku zote mtu hawezi kuona humuhimu wako ukiwa karibu nae unaweza ukasema kocha hana makosa hau uwongozi akuna yote kwa yote kupelekea kutaka timu hiwe kwenye ubora ila sizani kama Barcelona watasahau kazi yako uliyoifanya
Fatina mfigi
Duuh majanga kwa suarez
Mwajumah
Pole suarez