Nenda Yondani Ila Kumbuka Usaliti ni Kawaida

“Uzuri wa sura ulikuwa aula kweli, lakini ulikuwa si ufunguo wa kila kheri, ubaya wa sura ulikuwa dhila si uongo lakini ulikuwa si zuio la maendeleo, watu waliishi duniani kwa matendo yao siyo kwa sura zao, matendo ndiyo yaliyowatukuza au yaliwadunisha”. Shabaan Robert.

Nimemnukuu Mwanafasihi Hayati Shaban Robert, fumbua fumbo utalewa nini namaanisha! Wakati nakaa kijiweni wazee wangu na Mababu walikuwa wanataja sana jina la Salum Kabunda Ninja sikuwahi kumuona, walitaja jina la George Magere Masatu sikuwahi muona.

Waliniacha zaidi na zaidi waliponitajia Franco Baressi, Martin Kewon, Jaap Staam, Tony Adams bado nilikuwa gizani sana, kila wakitaja majina haya walikuwa wanasikitika sana, walibaki kujisemea dunia hii haina mabeki tena, dunia hii ina watoto laini sana.

Utasema dunia ina beki kama Salum Kabunda alikuwa anachukua mpira mdomoni mwa straika bila faulo?? Utasema dunia ina mabeki wakati Masatu anakuja kukukaba unasikia vishindo kama tembo?? Utasema dunia ina mabeki kama Jaap Stam sehemu ya mguu ataweka kichwa??

Watawezea wapi hawa vijana leo hii straika akifinya beki yupo chini, wangeweza kuendana na kasi ya Ronaldo de Lima?? Wangeweza kumzuia vipi Diego Maradona?? Dunia yenu haina mabeki hii tena, unamkumbuka Daniel Passarella,Allesandro Costacurta au Giacinto Faccheti??

Katikati ya stori zao wakamtaja Nemanja Vidic, hapo nikakaa vyema kwakuwa nimemuona huyu, Babu mmoja alisema Ulaya Mashariki napo kuna mabeki wakatili, Vidic kaishi kwenye moshi wa mabomu na anacheza mpira pembeni ya mizoga, si ajabu yeye kuwa mkatili, ni mtu haswaa.

Katikati ya maongezi wakamtaja Kelvin Yondan, walidai kuna kijana nchini anaitwa Vidic, hapo nilitamani kuwaambia Vidic yule hayupo tena kwa Young Africans, nilitaka kuwaambia kuwa Vidic ameondoka pale, ila kwenye mazungumzo yao walianza kupasifia Mwanza kuwa wana historia ya kutoa vitasa nchini.

Kijana mmoja mfupi sana, umbo dogo sana ambaye kwa macho unaona hasumbui, kwa hisia unaona ni uchochoro ila hiki ni kisiki, mtaani wanamuita Cotton, historia yangu inaanzia mbali sana jioni moja Kelvin Yondan na jezi ya Taifa.

Itaendelea….


Weka Pesa kwa Airtel Money!

Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!

Soma Zaidi

34 Komentara

    mambo ni moto na meridianbet

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Duuh hatari

    Jibu

    Habari imeeleweka

    Jibu

    Yondan skils za kufa mtu uhodar mkubwa hakuna beki kam huyu kutokea vpl

    Jibu

    Kumbe yupo huyu kiumbe

    Jibu

    Bye bye kelvin YOndani (COTTON) umri bado unatak ila mwili tatiz bye bye COTTON taifa stars itakumic Sana na wazee wa kkoo watakumisi sana

    Jibu

    Yondan skils za kufa mtu uhodar mkubwa hakuna beki kam huyu kutokea vpl

    Jibu

    yondani yupo makini sana awapo uwanjani ngoja nisubiri mwendelezo kuyajua zaidi kuhusu uyu nyota

    Jibu

    Yondan akiwa uwanjani anakuwa makini

    Jibu

    Inashangaza sana, Soka la bongo halina heshima

    Jibu

    Duhhhhh hii kali sasa

    Jibu

    Mmh kazi ipo

    Jibu

    Yondani nibek mzuri Sana anaejua kujituma kupambana nakuweka mchezo kwenye levo yake Sasa ngoja tuone kinacho jili tusikie mengi kwanyota huyo

    Jibu

    Tunawaombea kila la kheri wapambanaji wetu kila kitu kinaenda na wakati ule ulikua wakati wa (ottoni)yondani na wengine watatokea pia

    Jibu

    Yondani ni mchezaji mzuri tatizo yanga sijui wanakwama wapi

    Jibu

    Kwel kbs muhim umakin

    Jibu

    Kazi ipo hapo

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Tatizo la Yondani akishapitwa na mshambuliaji lazima acheze rafu #meridianbettz

    Jibu

    duh

    Jibu

    Namkubali sana pia hanaga kazi mbovu

    Jibu

    Mh nomaa

    Jibu

    Noma sana

    Jibu

    History yake Nd ilipoishia ana mpila sasa

    Jibu

    Yondan yanga ilimuach tu lakin ameondoka na mpira wake

    Jibu

    Kaondoka na mpira wake

    Jibu

    Mambo hayoo!

    Jibu

    Yondan mbn yupo vizuri

    Jibu

    Yondan anajitahidi sana

    Jibu

    hakuna beki kam huyu kutokea

    Jibu

    Yondani Ni mchezaji mzur ila lazima angalie maslai yake upandd mwingine

    Jibu

    Duuh kazi ipo apo

    Jibu

    Kipaji ichoo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.