Mwalimu Bielsa na Shetani au Malaika

Bielsa alichukua makaratasi na kuanza kumchorea baadhi ya vitu muhimu sana kutoka kwa Makocha mbalimbali, alimwambia kila kitu kuhusu Arrigo Sachi, Carlo Ancelotti, Mircea Lucescu wa Shakhtar Donetsk na Marcelo Lippi.

Baadae akamwambia “Mwanangu mimi ni Mzazi, nimewafundisha vijana wawili kuna wewe na Diego Simeone, mtaamua wenyewe kuwa wachawi au kuwa malaika” alimwambia hivyo kwakuwa aliwapa kila kitu kuhusu soka la kujihami na kushambulia, uamuzi ni wao

Bielsa hapendi soka la kujilinda ndio maana anapenda kumuita Simeone shetani na Pep Malaika kwakuwa anafunguka, alimaliza somo lake na kurudi na kijana wake nyumbani kwake, asubuhi Pep aliaga na akakbidhiwa kitabu maalum (Ipo siku nitaelezea kitu hiki).

Kumbuka Pep alipewa ahadi kuwa siku wakikutana tena amkute ameiva na anacheza kama alivyomwambia, ahadi yao ilitimia walipokutana Spain, Pep yupo na Barcelona na Bielsa na Bilbao, walikutana mara tatu, Pep alishinda mbili na sare moja, Mwanafunzi aliiva sana.

Kwanini watu wanamuita Bielsa Padre?? Kwa Kizungu wanamuita Priest of the Nun, hii ilitokana na baada ya kutimuliwa 2006 Ukocha Argentina akaamua akakae zake na Mapadre kutumikia tu jamii, hakutaka kujadili mpira kwa muda flani, ndipo hapo akapachikwa jina hilo.

Kwasababu za Kiafya, Bielsa aliambiwa akae mbali na mpira ili atazame afya yake kuanzia 2015, akarejea nyumbani kwake Buenos Aires kwenye mji wa Pwani ya Kaskazini Mashariki, ndipo hapo ikaja Leeds United kuhitaji huduma yake ila hawakuwa wanaamini kama Legend atakubali.

Simu ya Mmiliki wa Leeds, Adriazzini kuelekea kwa viongozi wa Victor Orta na Angus Kinnear iliwataka wasafiri mpaka Argentina kuonana na Mwalimu wa Pep baada ya Leeds kufanya vibaya 2017-18 Daraja la kwanza, baada ya Makocha wengi kufeli tu interview zao.

Baada ya maili 7,000 walifika kwa Bielsa, ajabu wanakutana na Babu aliekuwa anawafahamu wachezaji wote wa Leeds, anaifahamu mifumo yote ya timu 20 za Championship, El Loco aliwaambia haitaji usajli mpya bali watoto walewale, baada ya misimu miwili katwaa ubingwa na kuirejesha Leeds EPL.

Na huyo ndie El Loco Marcelo Bielsa, Mwalimu wa shetani na Malaika.


Weka Pesa kwa Airtel Money!

Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!

Soma Zaidi

29 Komentara

    Bielsa kocha makini sana ameweka rekodi nyingi tu

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Namuelewa kinyama

    Jibu

    Bielsa marcel ni bonge la kocha wa makocha

    Jibu

    Bielsa hapendi soka la kujilinda ndio maana anapenda kumuita Simeone shetani na Pep Malaika kwakuwa anafunguka, alimaliza somo lake na kurudi na kijana wake nyumbani kwake, asubuhi Pep aliaga na akakbidhiwa kitabu maalum (Ipo siku nitaelezea kitu hiki).

    Jibu

    kocha mwenye viwango vyake vya ajabu

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Nimeanza kuelewa kwanini Leeds wanaroho mbaya sana kumbe El Loco Marcelo Bielsa ni mtu mbaya sana, Namuona mbali kama Leeds wataedelea na form hii

    Jibu

    Bielsa ni kocha mzuri sana

    Jibu

    Bielsa ni kocha makini sana history yake haiwezi kufutika

    Jibu

    Yuko pouwa

    Jibu

    Bielisa ni kocha mwenye mfumo wake WA kipekee wa ufundishaji

    Jibu

    Namuerewa kocha Bielsa yupo vizuri Sana anaistoria kwenye soka kocha huyo

    Jibu

    Yupo vzr mbn

    Jibu

    Pamoja na mafanikio ktk soka lake anatakiwa kufikiria kuwa na mfumo wa kulinda goli maana timu yake inashinda lakini inaruhusu magoli mengi mno#meridianbettz

    Jibu

    Ila Yuko vizuri

    Jibu

    Yuko vizur

    Jibu

    Ni kocha mwenye histolia nzuri sana

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Yupo sahihi

    Jibu

    Mchawi wa soka la kushambulia kocha bielsa ana mpinzan

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Yuko vizuri sana

    Jibu

    Yupo sahihi

    Jibu

    Kocha anayejielewa

    Jibu

    Bielsa ni kocha mzuri

    Jibu

    Yupi vizur

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

Acha ujumbe