Joshua Kimmich alisema mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Bayern Munich walibahatika kuondoka na ushindi ugenini baada ya kuondoka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Lokomotiv Moscow.
Kimmich alifunga dakika ya 79 kukamilisha ushindi wa rekodi ya 13 mfululizo kwa Mabingwa wa Bundesliga na Mabingwa wa Ulaya, lakini nyota huyo wa Bayern alikiri kuwa ilikuwa ni bahati tu kutoboa pale dimbani RZD.
Goli la Kimmich liling’aa zaidi akipiga chapa mkwaju wa ushindi kutoka umbali wa takribani yadi 20.

Kimmich baadaye aliwasifu wapinzani wao juu ya mchezo huo.
“Nadhani Lokomotiv alikuwa na mchezo mzuri. Walikuwa wazuri katika kufanya mabadiliko, wakishambulia kwa wachezaji wenye kasi. Haikuwa rahisi hasa katika kipindi cha pili lakini mwishowe tulikuwa na bahati ya kuondoka na ushindi”
“Ulikuwa ushindi wa kweli. Hatukucheza vibaya, lakini tulipaswa kuumaliza mapema.
Kocha mkuu Hansi Flick alisifu mchezo wa Bayern na namna ambavyo walikuwa wakijiandaa mazoezini.
“Ilifanya kazi vizuri mara moja au mbili na ikatoka ikapata goli zuri. Ulikuwa ushindi uliopiganiwa kwa bidii, wenye kupendeza ukipenda. Moscow ilifanya vizuri, walilinda sana na walicheza na mipira mirefu, ambayo ilituumiza mara moja au mbili.”
“Lakini kwa jumla, nadhani tunaweza kusema ushindi wa 2-1 ulistahiliwa, hata ikiwa haikuwa wazi kama tunavyotarajia.”
Bayern bado hawajapoteza katika mechi 14 walizocheza ugenini Ulaya – katika historia ya Kombe la Uropa / Ligi ya Mabingwa ni Manchester United tu waliowahi kufikisha mechi (16) bila kufungwa.
Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.



aisha
Joshua mtu mbaya namkubali sana yuko vizuri
Hopemwaikuka
Hongeren sana
Fatuma kasomo
Gud
Dorophina
Walicheza vizuri bahati ilikuwa ni yao tu
Sauda
Joshua anajitahidi sana
Fatina mfigi
Pongezi kwako joshua kwa kazi nzur
Mwajumah
Hongera sana
Lydia Emmanuel Magoti
Pongezi zake
Tatu
Hongera yake
Ester jackson
Pongezi sana pia asante kwa nakala mana sikujua man u pia walikuwepo kwenye nafasi nzuri kipindi hicho
Sabrina
Hongera sana joshua
Elika
Safiiii sana
warda
Walicheza vizuri sana
Ernest
Bayern walicheza chini ya kiwango, Lokomotiv Moscow wangejitahidi wangeibuka na ushindi
Povel
Bayern Munich Wana ubora mkubwa Sana hata ingekuwaje bado wangepata matokeo tu