Uhaba wa washambuliaji unaendelea kuwatafuna Man City msimu huu. Gabriel Jesus na Sergio Aguero wanaendelea kuuguza majeruhi na hivyo Pep anakosa silaha zake za mashambulizi.

Kutokana na hali hii, Pep alinukuliwa akijutia kutosajili mshambuliaji katika dirisha la usajili lililofungwa mapema mwezi huu.

Aliyewahi kuwa mchezaji wa Man City – Micah Richards, anadhani timu hiyo inapoteza nafasi ya kumsajili mchezaji wao wa zamani [Daniel Sturridge] na pengine wanapaswa kumsajili kuziba mwanya huo.

Richards amenukuliwa akisema, “Ingekuwa rahisi kwa Daniel kuachana na soka lakini bado anahamu ya kufanikiwa.

“Mwaka jana alikwenda Uturuki kwa ajili ya kupata muda mwingi wa kucheza soka licha ya taarifa kuzagaa kwamba anaumia mara kwa mara. Alifanya vizuri akiwa na Trabzonspor kabla ya kufungiwa kwa kuvunja sheria za michezo ya kubahatisha.

“Kama atakujacheza tena soka basi itakuwa ni nje ya nchi lakini bado ninaamini kunatimu kwenye EPL bado zinahitaji huduma yake. Man City ninawaweka katika kundi hili. Kukosekana kwa Aguero na Gabriel ni nafasi kwa Sturridge kuwapa matokeo hata kama hatocheza msimu mzima.

“Kwa sasa ni kama watu wamesahau kabisa ubora wa Sturridge lakini bado anamuda wa kuwaonesha watu kiwango chake.” aliyasema haya wakati akiwa na Sky Sports kama mchambuzi wa soka.


TSH.160,000,000 KUSHINDANIWA!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Man City, Man City Wamsajili Sturrigde, MeridianbetKamata Mkwanja wako HAPA🤑

21 MAONI

  1. Wafanye tu mpango hata kwa gharama yoyote maana hali ya timu inapoelekea sio pazuri kukosa washambuliaji ni hatari kwenye timu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa