Liverpool wanaendelea kupitia wakati mgumu katika kikosi chao msimu huu baada ya Fabinho kuumia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa.
Akiwa anaziba pengo la Virgil Van Dijk ambaye atakua nje kwa muda mrefu, Fabinho aliumia katika dakika ya 30 ya mchezo huo dhidi ya Midtjylland.
Majeruhi kwa Fabinho ni pigo kwenye kikosi cha Liverpool kwani huenda wakamkosa mchezaji mwingine wa muhimu kwenye kikosi hicho. Hatari kubwa itakuwa kwenye safu ya ulinzi wa timu hiyo ambayo inauhaba wa walinzi wa kati.
Kocha – Jurgen Klopp, amezungumzia suala hilo “sijajua hali itakuwaje lakini aliumia kwenye paja.
“Alisema hajaumia sana na angeweza kucheza ila lakini asingeweza kukimbia kitu ambacho kwa kiasi fulani kisingesaidia. Tutaliangalia hilo, atafanyiwa vipimo ila hali si nzuri.” aliyasema haya kupitia BT Sport.
Licha ya Fabinho kutolewa katika dakika ya 30, Liverpool waliibuka na ushindi wa magoli 2-0 katika mchezo huo.
Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.



aisha
Duuuhhh majanga kwa klopp mungu tuu awasaidie maana wanapitia kipindi kigumu sana sijajua itakuaje
Hopemwaikuka
So sad to them
Fatuma kasomo
Duh pole yao
Dorophina
Klopp anazidi kuandamwa na majanga tu itafikia hatua watashuka daraja
Sauda
Poleni sana Liverpool
Fatina mfingi
Polen
Mwajumah
Pole yao
Lydia Emmanuel Magoti
Duu pole yao Liverpool kwamajerui kuongezeka
Tatu
Liverpool wameaza msimu vibaya
Ester jackson
Kivumbi kimewageukia Liverpool sana hemea joto la jiwe sasa
Sylvester
Klop itabidi ajipange upya kutokana na majeruhi wanaoendelea kupatikana klabuni hapo
Sabrina
Apambane tu klopp anajinsi kujipanga
Khadija
Asnte kwa taarifa
Elika
Pole kwa Liverpool
warda
Hatari sana na pole yao
Mwanahamisi
Pole yao
Amani Maeda
Kuna uwezekano mkubwa wa Liverpool kuchezea kipigo tena.
Povel
Duh majanga kwl ndani ya Anfield