Nyota wa Liverpool Trent Alexander-Arnold alifurahia mafanikio makubwa ya kilabu wakiwa wanasherehekea bao lao la 10,000 katika ushindi wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Midtjylland.
Mkwaju wa Diogo Jota uliwasaidia Liverpool kushinda 2-0 nyumbani kwa Midtjylland, lakini pia uliwapa Liverpool bao la kihistoria kwa mashindano yote.
Mabingwa wa Ligi ya Premia Liverpool walifikisha miaka 128 tangia kufunga bao lao la kwanza – ikiwa ni juhudi za Jock Smith katika ushindi wa 8-0 dhidi ya Higher Walton huko Anfield kwenye Lancashire League.
Alexander-Arnold alitoa pasi ya usaidizi wa goli dakika ya 55 na Jota akaandika bao la kwanza kabla Mohamed Salah hajafunga hesabu kuondoka na alama za Kundi D kwa mkwaju wa penati.
Alexander-Arnold akisifu goli la Jota alisema lilikuwa goli zuri sana, zaidi akasema ushindi na kujivunia mafanikio ni historia nzuri ya klabu. “Tuna historia ya kujivunia na ni mafanikio makubwa kufikia alama hiyo.”
Bao la Jota lilikuwa la 370 Liverpool wamefunga kwenye mashindano ya Klabi Bingwa Ulaya, na magoli 6,968 wameyapata katika Ligi Kuu Uingereza
Magoli mengine ni kwenye daraja la pili (mabao 977), na Kombe la FA (708) na Kombe la EFL (481), wakati Liverpool imefunga mabao 371 kwenye Ligi ya Mabingwa.
Mashindano mengine mashuhuri ni pamoja na Kombe la UEFA / Ligi ya Uropa (173), Kombe la Dunia la Klabu (6) na Ngao ya Jamii (26).
“Baada ya ushindi mzuri ugenini, ni muhimu kuendelea kuongeza alama na tulifanya kazi yetu. Tunapata alama tatu, hiyo ni muhimu zaidi, na sasa tunahitaji kuwa tayari kwa mchezo ujao.” -Alexander-Anorld
Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.



aisha
Jamani hiyu Alexender anasitahili pongezi sana pia sidhani kama kuna mchezaji wowote ambaye anamfikia kwa magoli
Hopemwaikuka
Waooo! Mmetisha sanaa
Fatuma kasomo
Safi sana
Dorophina
Pongezi kwa liverpool
Sauda
Liverpool jitihada zenu zinaonekana kwa kweli
Fatina mfigi
Mnastahil pongezi liverpool kwa kazi nzur mnanyo ifanya!!
Mwajumah
Safi sana
Lydia Emmanuel Magoti
Duuu kweli shangwe magoli Elfu 10,000 sio poa pongezi zake kiungo mshambuliaji
Tatu
Liverpool wanajitihada sana kwenye soka
Ester jackson
Good
Sabrina
Inapendeza sana
Elika
Safiiii sana
warda
Hata mie Ningefurahia
Ernest
Alexander-Arnold bado ananafasi ya kuendelea kuwa mwiba ndani ya Liverpol kutokana na style ya uchezaji wake.
Povel
Congar kwake Arnold Alexander’s