Barcelona: Hatimaye Raisi Ajiuzulu, Bodi Inamfuata!

Jumanne, Raisi wa Josep Maria Bartomeu alitangaza mpango wake wa kujiuzulu kama rais wa Barcelona.

Bartomeu ambaye ana umri wa miaka 57 alithibitisha kuwa yeye na bodi nzima ya wakurugenzi wangeachia ngazi kabla ya kuepuka kura ya kutokuwa na imani iliyopangwa kufanyika katika ofisi za Camp Nou wikendi hii.

Bartomeu tayari ametoa hotuba kwa waandishi wa habari, wanachama na mashabiki -Juu ya sakata zima na mamuzi yake ya kuachia ngazi.

Katika hotuba yake, raisi amesisitiza kuwa uamuzi huo ni baada ya kujitahmini na kufanya majadiliano ya kina na bodi ya wakurugenzi klabuni hapo.

“Huu ni uamuzi unaofikiriwa vizuri, kwa utulivu, na makubaliano ya pamoja na wakurugenzi wenzangu ambao wameandamana nami kwa miaka ya hivi karibuni kwa uaminifu na kujitolea kuhusiana na miradi na kilabu, na ambao wamejitoa mhanga sana kufikiria kila wakati kwa ajili ya Barcelona.” -Sehemu ya hotuba ya Bartomeu

Katika hotuba yake ya kuachia ngazi ametaja mambo mengi sana, lakini kubwa ni kuwa hawawezi kusubiri kura ya kutokuwa na imani nao ipigwe hasa katika kipindi kama hiki cha Corona ambacho suala la afya linapaswa kupewa kipaumbele.

Bodi inayoachia ngazi, inaamini kuwa Barcelona itakuwa kwenye mikono salama ya bodi ya mda, ambayo bila shaka kutokana na hali halisi ya afya, haitaweza kuendesha zoezi la upigaji kura hivi karibuni.


 

Tsh.160,000,000 Kushindaniwa!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Kamata Mkwanja wako HAPA

14 Komentara

    Bora hata alivyojiudhuru maana angesubilia kura za maoni angeondoka kwa aibu amna kazi yoyote wanayoifanya Barca timu inazidi kuyumba

    Jibu

    Matokea ulshatoa mabaya sio vbaya ulivyojiuzuru tu

    Jibu

    Jamaaa kaogopa wajumbe maana wajumbe sio watu wazuri wangemtimua

    Jibu

    Amejitoa mapema sana.

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Duu kafanya haraka Sana kujiuzuru atakama matokeo kutoka vibaya ndio ivyo Sheria lazima ifatwe

    Jibu

    Bora alivyojitoa

    Jibu

    Bora aondoke tunataka mambo mazuri sisi

    Jibu

    Duuh hatari sana

    Jibu

    Hatar hiyo

    Jibu

    Jamani kafanya maamuzi magumu sana

    Jibu

    Umefikia wakati wa Barca wa kumtafuta mchawi nani, Ngoja tuone mpasuko mwingine mkubwa

    Jibu

    Habar mbaya kwa mashabik wa barcelona

    Jibu

Acha ujumbe