Waswahili husema ‘nabii hakubaliki nyumbani’. Ukitaja Bruno Fernandes ukiwa Ureno, sio wengi watakaoshtuka kama utakavyosema Cristiano Ronaldo. Ila mtaje Fernandes ukiwa Manchester na utapigiwa makofi kwa shangwe kubwa kutokana na uwezo wa kiungo huyo.
Bruno Fernandes afunguka kuhusu kumpatia Marcus Rashford penati licha ya kwamba ilikuwa ni nafasi yake kupachika ‘Hat-trick’ kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na Man United.
Mchezo wa 4 kwenye hatua ya makundi kunako Ligi ya Mabingwa, Man United walikutana na Istanbul Basaksehir katika mchezo wa marudiano baada ya kupoteza mchezo wa kwanza.
Alikuwa ni Bruno Fernandes aliyepeleka shangwe kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kupachika magoli 2 ndani ya dakika 20 na mchezo ulimalizika kwa ushindi wa 4-1.

Bruno Fernandes alikuwa na nafasi ya kupachika goli la tatu lakini aliamua kumuachia Rashford jukumu la kupiga penati kunako dakika ya 35 na muingereza huyo hakufanya makosa, alipachika goli la 3.
Akizungumzia uamuzi huo, Fernandes amesema “ni kweli kila mchezaji anataka ‘hat-trick’ lakini baada ya mchezo wa EPL (dhidi ya West Brom) nilimwambia Rashford atapiga yeyote itakayofuata.
“Lakini pia ni miongoni mwa wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa kwa hiyo ni muhimu kwake kuendelea kujiamini zaidi.
“Haijalishi ni nani anapiga penati, kitu cha muhimu ni ushindi”
Kocha Ole Gunnar Solskjaer naye alikuwa na chakusema kuhusu uamuzi wa Fernandes. Ole amenukuliwa akisema “Marcus ni mpigaji mzuri wa penati na Bruno anajiamini sana, kama Bruno alitaka kumpatia Marcus sasa kwanini asifanye hivyo? Anthony Martial alipiga kwenye mechi dhidi ya Leipzig – sasa kwanini wasishirikiane?
Huu ni mchezo wa kwanza kwa United kuongoza kwa magoli 3 kabla ya mapumziko kwenye Ligi ya Mabingwa. Mara ya mwisho walifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Roma (7-1) mwezi Aprili, 2007.
Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.



magdalena
fernandes yupo vizuri sana ata wasipomkubali kwao potelea pote sisis mashabiki tunaangalia ni nini anafanya
Sauda
Fernandes anastahili pongezi maana magoli 2 ndani ya dakika 20 si mchezo.
Shakila mrope
Hatari san
Dorophina
Fernandes anajua nini anafanya katika klabu yake ndiomaana man u wanamuamini sana
Mwajumah
Namkubali sana uyu jamaa Fernandes kwan anajua kulisakata soka vizuri tu
Ester jackson
Kitu muhimu in utendaji wa kazi
Adelta
Fernandes Yuko vizuri pongezi kwake
Angelina
Safi Fernandez
Caroline
Fernandez anajua nini anafanya..
Sania
Vizur sana Fernandez
Rahma
Fernandez Yuko poa
Khadija
Asante kwa taarifa
Fatina mfingi
M2 Makin sana!!
Hopemwaikuka
Fanya kwa nafas yako
aisha
Sisi mashabiki tunakubali kazi yake kwenye mpira
Povel
Fernandez ni mmoja wachezaj muhimu ndani ya manchester united hv sasa
Saupha mohamed
Vizuri sana
Issa
Bruno amekua mtu makin na ameleta morali sana man u
Gabriel
Nice upadate 👍
Sadick
Man U imekuwa ikipata penati karibia kila mchezo jambo ambalo linashangaza wengi. Bruno ni mpigaji mzuri wa Penati na alikuwa muungwana kumwachia mwenzie
samiah
Nice
Latifa juma mohamed
Hatari yake.
Tatu
Kijana yupo vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Kijana anajua
Sarah
Yuko vizuri
warda
Bruno anajua bwana