MABINGWA wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al-Ahly ya Misri, jana usiku Novemba 27 wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa tisa baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wa Zamalek.
Zamalek ambao hawajatwaa ubingwa tangu walipovuliwa na Simba mwaka 2003, walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Suyala dakika ya 5, Al-Ahly walisawazisha bao hilo dakika ya 39 likifungwa na Shikabala.

Wakati wengi wakiamini kuwa mechi hiyo ya ‘Cairo Derby’ watashuhudia dakika 120, mchezaji wa Al-Ahly, Ashfa, aliweka kambani goli la dakika ya 88 ambalo liliwahakikishia ubingwa.

Kocha wa Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane, ametwaa taji lake la pili la klabu Bingwa Afrika baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza 2015/2016 akiwa na Mamelodi Sundowns ya kwao Afrika Kusini.
Baada ya kuiwezesha Al Ahly kutwaa taji la tisa la Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kukaa na ukame kwa miaka saba, inaarifiwa kuwa Pitso atapewa bonasi ya dola za Marekani 500,000 (Tsh Bilioni 1.1).

Pitso anaingia katika rekodi ya kuwa kocha wa tatu aliyewahi kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili akiwa na timu mbili tofauti.
Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.



Adelta
Good news 👍😃
Dorophina
Pongezi kwao
Magdalena
Jambo jema sana
Asia Abdy
Kwa Africa hawana mpinzan
Sauda
Hongera yao
Ester jackson
Pongezi kwao
Issa
Wababe wa africa
Hopemwaikuka
Congratulations to them
Fatina mfingi
Nice
Tatu
Pongezi kwao
Janeflora malisa
Safi
Shafii
Wanastahili pongezi
aisha
Safi sana kwa kupeperusha bendera ya Africa
Nasra
Pongezi
Rahma
Saf
warda
Mwisho wao umefika ngoja Simba achukue mwakani