Wakala wa nyota wa Manchester United Paul Pogba, Mino Raiola ameonekana akiwa Turin katika kipindi ambacho nyota huyu wa Manchester United anahusishwa zaidi na kurejea Juventus.
Sio siku nyingi zimepita tangia meneja huyu aweke wazi kuwa mda wa Paul Pogba kuwepo Manchester United tayari umeisha. Lakini pia alisistiza kuwa kutokana na hali ya dirisha la uhamisho, sio rahisi sana kukamilisha uhamisho mapema, na atalazimika kusubiri hadi mwisho wa msimu.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari za michezo nchini Italia, wakala Mino Raiola ameonekana akiwa mjini Turin. Hii imefufua matumaini ya mashabiki wa Juventus ambao wamekuwa wakitamani staa huyu kurejea. Hata hivyo, bado mpango mzima haujawekwa wazi ikiwa suala la Pogba ndiyo lililompeleka Turin.
Ikiwa Juventus wataitaka saini ya Pogba, mazungumzo ya kukamilisha dili hili yanatarajiwa kuwa yatakuwa magumu kidogo kwa sababu klabu hiyo inaweza ikalazimika kuwauza wachezaji kadhaa kuwa katika nafasi nzuri ya kukamilisha uhamisho wa Pogba.
Sehemu ambayo inaonekana kuwa itakuwa ni changamoto zaidi ni kumshawishi Pogba kukubali punguzo la mshahara. Pia kukubaliana na Manchester United wakubali kumuuza kwa mkopo kwa chaguo la kumnunua baadaye.
Hapa lazima pawe patamu! Tuambie wewe una mtazamo gani, Pogba arejee Juventus?
BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!



Hopemwaikuka
I think anaweza kwenda
Adelta
Kama ameshaamua lazima aondoke tu
Alafu maisha mengine yaendelee manchester united
warda
Aende tu mie naona kama anachelewa kuondoka
Rahma
Mamuzi anayo yeye Kama anataka kusepa asepe akili kichwan mwake
Sarah
Nibora aende tu km ameamua kuondoka
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri uwamuzi niwake
Mwanahamisi
Ni bora aende tuu
Saupha mohamed
Maamuzi yake
Tatu
Popote kambi
samiah
Kambi popote