Ronald Koeman: Hali ya Hewa Iko Poa Barcelona!

Kocha wa Barcelona, Ronald Koeman anasema kuwa hali ya hewa iko shwari kabisa kwenye kikosi chake na wakati wote  wachezaji wake wamekuwa na mtazamo chanya.

Barca wapo nyuma kwa pointi sita dhidi ya vinara wa ligi Atletico Madrid, wakiwa tayari wamepoteza mechi 4 kati ta mechi zao 12 chini ya Koeman ambaye alichukua nafasi ya Quique Setien.

Barca walipokea kichapo kutoka kwa wapinzani wao Real Madrid na Atletico, pia walipata kichapo kilichowashangaza wengi kutoka kwa Getafe na Cadiz.

Hata hivyo, walionesha kuboreka katika mecchi yao dhidi ya Real Sociedad ambayo walipata ushindi wa 2-1. Koeman anasema kikosi chake kipo shwari na mipango zaidi ni kuendelea kupata ushindi.

Kutokana na hali halisi ya klabu kwa sasa, baadhi walikuwa wanaamini kuna walakini kwenye hatma ya meneja huyu, lakini yeye anawaondoa hofu waliyopo nyuma yake kuwa mambo yapo shwari.

“Wakati wote nimeona hali shwari, licha ya mechi tulizopoteza. Ni rahisi kuwa na hali ya furaha ukiwa umeshinda.”

Mpango wa Koeman, ambao amesisitiza zaidi ni kuendelea kufanya mabadiliko chanya katika kikosi na kuendeleza ushindi. Wanaelekea kuingia dimbani Jumamosi hii dhidi ya Valencia, hii ni fursa ya kuthibitisha namna anavyokipamba kikosi chake.


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

11 Komentara

    Ni jambo jema

    Jibu

    Koeman anajitahidi kikosi kikae sawa

    Jibu

    Naamini Koeman atafanya vizuri sana badae

    Jibu

    Abali njema

    Jibu

    Jambo jema

    Jibu

    Barca kwa sasa inamatumaini makubwa

    Jibu

    Barca inakaa sawa

    Jibu

    Vizuri Barcelona Mambo yashakuwa mazuri sasa

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Good news

    Jibu

Acha ujumbe