EPL: Nyepesinyepesi Kutoka kwa Makocha.

Kuekelea wiki ya 14 ya Ligi Kuu Soka nchini Uingereza – EPL, ni utaratibu wa kila kocha au meneja wa timu kuzungumza na waandishi wa habari kabla na baada ya mechi zao.

Tuziangalie habari nyepesinyepesi kutoka kwa baadhi ya makocha wa EPL ambao wameshazungumza na waandishi wa habari hadi kufikia muda huu.

Mikel Arteta atasafiri na kikosi cha Arsenal kuwafata Everton wikiendi hii. Mchezo huu utachezwa siku ya Jumapili ambapo Arteta atakuwa anatimiza mwaka 1 tangu akabidhiwe mikoba ya kukinoa kikosi hicho.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta.

Kwa ufupi sana, Arteta amegusia kutokufurahishwa na muenendo wa timu yake kwa sasa lakini pia amesisitiza kuwa sio jambo la haraka haraka katika kuirudisha Arsenal inapotakiwa kuwa.

Mikel Arteta amesema “Kwenye ulimwengu wa soka unahitaji matokeo lakini baada ya mabadiliko makubwa tunahitaji uwiano. Tunahitaji muda na kwakulitambua hilo, maamuzi ya kunikabidhi hili jukumu yalifanyika. Hayakuwa maamuzi ya kukurupuka na itachukua muda, unapobadilisha vitu lazima utumie muda kurejea ulipokuwa.”

Jurgen Klopp atawaongoza mabingwa watetezi wa EPL – Liverpool kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace. Kati ya vingi alivyogusia kocha huyu, ameongelea tuzo yake ya FIFA (Kocha bora wa wanaume) pamoja na hali za wachezaji majeruhi.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.

Klopp amesema “Nimeshukuru kwa hilo (kupata tuzo) lakini kama watu wengine tu (nilishangaa), sikuwa ninaitegemea. Nilidhani Kocha wa Bayern Munich [Hansi Flick] alishinda kila kitu mwaka jana.”

Kuhusu maendeleo ya wachezaji wanaopambana na majeruhi, Klopp ameeleza kuwa Thiago Alcantara anaendelea vizuri na ameanza mazoezi madogomadogo. Japokuwa, hatomuharakisha kurejea uwanjani. James Milner na Xherdan Shaqiri pia wanaendelea vizuri kiafya.

Steve Bruce ataiongoza Newcastle kwenye mchezo dhidi ya Fulham. Newcastle walikumbwa na madhila ya maambukizi ya COVID19 miongoni mwa wachezaji na wafanyakazi wa klabu hiyo.

Kocha wa Newcastle United, Steve Bruce.

Bruce anaona matumaini mapya kwenye kikosi chake licha ya kwamba anauwezekano wa kuwakosa wachezaji 4 au 5 kwenye mchezo huo kutokana na maradhi. Habari njema kutoka Newcastle United ni kwamba hakuna majeruhi wapya baada ya mchezo waliopoteza dhidi ya Leeds United mapema wiki hii.

Chris Wilder alitoa taarifa fupi kuhusu timu yake ya Sheffield United ambao walipoteza mchezo dhidi ya Man United jana usiku (3-2). Sheffield watachuana na Brighton Albion katika mchezo ambao Wilder amethibitisha hali ya sintofahamu kwa Oli McBurnie na Sander Berge ambao waliumia kwenye mchezo dhidi ya United.

Kocha wa Sheffield United, Chris Wilder.

EPL itaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali wikiendi hii mechi ya kwanza ikiwa ni Crystal Palace dhidi ya Liverpool, kesho Jumamosi majira ya saa9:30 alasiri.

Mchezo wa mwisho kwa wiki ya 14 ya EPL utachezwa Jumatatu saa5 usiku, Chelsea wakiwakaribisha West Ham United.


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

17 Komentara

    Hii itakuwa ngumu kumeza ngoja tusubiri matokeo tuone

    Jibu

    tusubirie matokeo

    Jibu

    saf

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Pamenoga ngoja tuone matokeo kwamechi zote hizo

    Jibu

    Mmh hii ni ngumu

    Jibu

    Mhh hatari tusubilie matokeo

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Eeh

    Jibu

    Arsenal vs Everton ni bonge la mechi

    Jibu

    Arteta wachezaj wako wanazingua sana

    Jibu

    Utaratibu wao uko poa sana

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Epl kumenoga

    Jibu

    Safi Epl

    Jibu

Acha ujumbe