COVID19 Inaiweka EPL Mashakani.

Hali sio shwari nchini Uingereza hii ni baada ya matokeo ya vipimo vya COVID19 kuonesha ongezeko kubwa la waathirika kwenye EPL na nchi hiyo kwa ujumla.

Taarifa iliyotangazwa jana (Jumanne) ilionesha idadi ya wachezaji pamoja na wafanyakazi wa vilabu mbalimbali ambao wamekutwa na virusi vya COVID19 ni 18.

Taarifa ya hii inahusiana moja kwa moja na baadhi ya michezo ya EPL kughairishwa ikiwa ni pamoja na mchezo wa Manchester City dhidi ya Everton. Pia klabu ya Fulham imeripoti visa vipya vya virusi vya Corona na hivyo mchezo wao dhidi ya Liverpool leo usiku upo mashakani.

Ni nini kifanyike ili kukabiliana na mlipuko wa COVID19?

Baadhi ya makocha wametoa maoni yao kuhusu muendelezo wa EPL, EFL na michezo kwa ujumla.

Sam Allardyce

Kocha wa WestBrom Albion – Sam Allardyce baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Leeds (5-0) aligusia suala hili kwa kusema ” Usalama wa kila mmoja ndio kitu cha muhimu zaidi. Licha ya kwamba tunapimwa kila mara, bado tulipata muathirika mmoja.

“Haijalishi tunajaribu kujilinda kwa kiasi gani, tunatumia vitakasa mikono mara ngapi, tunatumia barakoa kiasi gani, bado tunaendelea kuathirika kila kukicha.

“Kama kusimamisha ligi ndio njia sahihi ya kupambana na hili, basi iwe hivyo. Ni kheri msimu uwe mrefu lakini tulishinde hili.”

Ole Gunnar Solskjaer

Kocha wa Man United – Ole Gunnar Solksjaer kwa upande wake anasema ” kama klabu, tumekuwa tukizingatia zaidi utaratibu uliowekwa. Hiyo ni sehemu ya kazi yetu.

“Sioni sababu ya kusimamisha msimu kwa sababu ni lini tutaendelea kucheza michezo iliyobaki?

“Sote tunajua huu ni mwaka mgumu lakini kama unakwenda kusimamisha msimu, sidhani kama itakuwa na tofauti kubwa – utakuwa ni msimu mrefu na ni lini msimu huu utaisha?”

Ukiwa kama mdau wa michezo, unadhani ni kipi kifanyike katika hili??


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

19 Komentara

    Mbona balaa hili jamani

    Jibu

    Wazidi kuchukua tahadhari

    Jibu

    Corona sio poa

    Jibu

    Yatapita mana sio poa

    Jibu

    Colona hatari

    Jibu

    Corona noma

    Jibu

    Colona inatisha sanq

    Jibu

    Tuombe Mungu ipite iyo corona

    Jibu

    Majanga haya

    Jibu

    Corona ishakuwa tishio ndani ya Epl

    Jibu

    Corona ni janga kubwa dunian

    Jibu

    Corona ishakuwa tishio ndani ya Epl

    Jibu

    Hatari sana

    Jibu

    Hatar snaa

    Jibu

    Duuu atariii hii

    Jibu

    Corona ni hatari kwa dunia

    Jibu

    Coronavirus sio poa

    Jibu

    Duuh hatari

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.