Tetesi za Soka Barani Ulaya.


 

Tetesi zinasema Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Real Madrid Isco, 28, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa.

Kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ataamua wiki hii iwapo atatia saini kandarasi mpya na klabu ya Liverpool huku kocha wa Barcelona Ronald Koeman akiwa na matumaini ya kumshawishi kiungo huyo kujiunga na Barcelona.

Manchester City boda ina matumaini itamsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi 33, mwaka 2021, licha ya nahodha huyo wa Barca kusema kwamba anatumai kwamba siku moja atacheza soka nchini Marekani.

 

Mauricio Pochettino anatarajiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji wa Tottenham ikiwemo kiungo mshambuliaji Dele Alli, 24, na kipa wa Ufaransa Hugo Lloris, iwapo kocha huyo raia wa Argentina atathibitishwa kuwa mkufunzi Paris-St Germain.

Wolves huenda ikawasilisha ombi la kumsajili Diego Costa, 32, kuchukua mahala pake mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29, baada ya mshambuliaji huyo wa Uhispania kukubali kusitisha kandarasi yake katika klabu ya Atletico Madrid na kuwa mchezaji huru mwezi Januari.

Tetesi zinasema Tottenham inataka ya kumsajili kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer, 26, mwezi Januari kulingana na klabu yake RB Leipzig.

Tetesi zinasema Arsenal imesitisha mpango wa kumnunua mchezaji wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa.

 

Houssem Aouar
Houssem Aouar

Tetesi zinasema Liverpool imesitisha mpango wa kumsajili beki wa kati wa Inter Milan Milan Skriniar, 25, baada ya kukasirishwa na dau la £54m lililowasilishwa na klabu hiyo ya Italia.

Beki wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 30, anatarajiwa kurudi Uhipania na kujiunga na Atletico Madrid kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari . Alonso hajaichezea Chelsea tangu tarehe 26 Septemba.

Mkufunzi wa zamani wa England na Juventus Fabio Capello anasema kwamba atabadilishana mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27,na mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

17 Komentara

    Wajitahidi watampata

    Jibu

    Sijui kama mess atakubali kwenda man city

    Jibu

    Mmmh sio kweli messi kutoka hapo alipo

    Jibu

    Mess akomae

    Jibu

    Mess bora awadindie asichomoke kwenda kokote

    Jibu

    Mess hawezi kutoka hapo

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Mmmhhh mess kutoka awezi ila sijui

    Jibu

    Juve fanyen huo mpango

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Ni hekaheka tu za usajili

    Jibu

    Imekaa poa snaa

    Jibu

    Zipo poa

    Jibu

    Messi atulie na timu yake

    Jibu

    Messi hapo kashafika

    Jibu

Acha ujumbe