Kocha Mkuu wa Klabu ya FC Platinum Norman Mapeza amesema kuwa anawatambua wapinzani wake Simba vizuri hawampi presha atawasumbua ndani ya uwanja na kupata matokeo.
FC Platinum wametia timu leo Januari 2, Dar es Salaam na kupokelewa na uongozi wa timu hiyo ambao uliwahi mapema kuweka kambi ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Kwenye mapokezi ya leo hakukuwa na mashabiki waliojitokeza wakiwa na jezi za rangi yoyote tofauti na mapokezi ya timu ya Plateua United.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mapeza amesema kuwa wachezaji wapo vizuri na wanaamini watalinda ushindi na kupata ushindi ugenini.
“Tumekuja kwa kazi moja ya kutafuta ushindi hakuna jambo jingine ambalo tunahitaji hivyo wapinzani wetu wajiandae kisaikolojia tunawatambua, tunawaheshimu ila hatuwaogopi,” amesema.
Mchezo wa kwanza uliopita FC Platinum ilishinda bao 1-0 dhidi ya Simba Januari 6,Uwanja wa Mkapa ikiwa itashinda ama itapata sare inapenya hatua ya makundi.

Simba inatakiwa ishinde mabao zaidi ya mawili ili iweze kusonga hatua ya makundi.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?



Adelta
Mashabiki tunamkaribisha Sana tunasubiri tuone maajabu yake
Caroline
Akae kwa kutulia
Chiku
Yani asiwe na haraka
Dorophina
Tunasubilia iyo siku tuone maajabu yake
Mwanahamisi
Tunangojea kwa hamu
Neema juma
Maajabu tunayasubiriaaa
Saupha mohamed
Tunasubili kwa hamu
Devotha
Tunamkaribisha sana
Hopemwaikuka
Atajua ajui
Lydia Emmanuel Magoti
Tunasubili mahajabu yafanyike sio maneno tunataka vitendo
Angelina
Hana maajabu
Magdalena
Tunasubiri kuona maajabu yake
warda
Sijui itakuwaje hiyo tar. 6 ila naiombea sana Simba ushindi wa nguvu
Rahmal
Majabu akuna tunangojea tuone
Ernest Kimeru
Ngoja tuone
Sania
Tunataka tuone vitendo
Issa
Watakalishwa
Sabrina
nasubiri nijionee