Zidane Hana Mpango wa Kumpumzisha Benzema.

Zinedine Zidane hana mpango wa kumpumzisha mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema kwani alisema atamchezesha Eden Hazard kidogo kidogo ili arejee kwenye mchezo kamili.

Benzema alishindwa kupiga shuti hata moja langoni katika ushindi wa 2-0 wa Madrid dhidi ya Celta Vigo kwenye LaLiga siku ya Jumamosi.

Mchezaji huyo wa miaka 33 ameanza katika mechi 15 kati ya 17 za LaLiga msimu huu ni kipa Thibaut Courtois pekee na Raphael Varane wamecheza dakika nyingi zaidi yake.

Alipoulizwa katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi ikiwa Benzema, ambaye amefunga mabao nane katika LaLiga, atahitaji kupumzika, kufuatia kiwango kidogo alichoonesha, Zidane hakukubali.

“Sidhani kama amechoka,” Zidane alisema.

“Nadhani alifanya vizuri na nikamchukua ili mchezaji mwingine acheze. Tuko katika uelekeo mzuri. Tunafanya vitu sahihi na lazima tuendelee hivi.”

Hazard alitokea benchi katika mchezo huo katika kipindi cha pili cha mchezo na ulikuwa mchezo wake mwingine baada ya kutoka kuuguza majeraha

“Tutakwenda kidogo kidogo,” aliongeza Zidane. “Kidogo kidogo, lazima urejeshe hisia.

“Polepole na sio kulazimisha chochote. Lazima arudi kwenye ubora wake na aichukue polepole. Ni hayo.”


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

14 Komentara

    Maamuzi mazuri

    Jibu

    Benzema yupo vizuri

    Jibu

    Muache apge kaz

    Jibu

    Safiii benzema yupo vizuri

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Benzema yupo vizuri lazima apige kazi mwanzo mwisho

    Jibu

    Benzema noma

    Jibu

    Wamuache apige kaz

    Jibu

    Benzema Yuko makini

    Jibu

    Zidane huwa anamkubali sana benzema

    Jibu

    Beneza Yuko vizuli

    Jibu

    Ngoja tuone

    Jibu

    Benzema bado yupo fiti

    Jibu

    Benzema hafai

    Jibu

Acha ujumbe