Kocha mkuu wa timu ya taifa ya DRC, Florent Ibenge Ikwange, amesema hakuwahi kuwa na maambukizi ya virusi vya corona, lakini alilazimishwa kukaa karantini.
Akiongea baada ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa wenyeji Cameroon kwenye robo fainali hapo jana, Ibenge alilalamikia mbinu chafu ya wenyeji kuwavuruga kisaikolojia.
Nililazimishwa kutumia dawa ilhali sikuwa nikiumwa. Sikuwa na COVID -19, lakini walisema ninao. Hivi siyo vizuri. Na siyo mimi pekee.
Nina wachezaji ambao hawakucheza hata mechi, ambao pia hawakuwa na maambukizi lakini wao walisema wanayo.

Hii siyo hali ya kawaida. Mpira ni furaha na siyo kuua watu.
Kabla ya mchezo dhidi ya wenyeji Cameroon, kulikuwa na utata mkubwa kwenye kambi ya DRC kuhusu COVID -19.
Wachezaji 13 wa DRC walikutwa na maambukizi mapya, na kufanya kuwa na jumla ya maambukizi 25 pamoja na yale ya mwanzo.
Wakongo wakapinga sana majibu haya ya vipimo na ikabidi vipimo vichukuliwe upya, wachezaji wawili tu na kiongozi mmoja, ndiyo wakabainika wana maambukizi.

Jana (juzi) majibu yalikuja yakionesha wachezaji wetu 13 wana maambukizi ya COVID-19.
Tukapinga na kuomba vipimo vichukuliwe upya. Majibu ya pili yakaja leo (jana) ambapo ni watu watatu tu ndiyo walikuwa na maambukizi, wachezaji wawili na kiongozi mmoja. Hii ni picha mbaya sana kwa Cameroon.
DRC imewakosa wachezaji wake muhimu kwenye mashindano haya, kama Issama Mpeko, Kinzumbi Philippe na wengine ambao hawakucheza hata mechi moja tangu wawasili kwenye ardhi ya Cameroon, kutokana na kuonekana kuwa na COVID-19.

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!



Khadija
Jamani corona balaaaa
Adelta
Coronavirus sio poa
Caroline
Hii corona ni mchezo wa mabeberu..
Sania
Dah corona sio poa
Lydia Emmanuel Magoti
Duu Corona sio poa
Magdalena
Pole yake iyo ndo changamoto ya mafanikio
Venerose
Kwenye game Mambo kama hayo yapo
Mwanahamisi
Corona inatisha
Sarah
Duu corona noma sana
Hopemwaikuka
Mapya haya
Dorophina
Duu hili balaa changamoto za wapinzani hizo
Rahmal
Ibenge pole sana
warda
Corona itakuja kufanya watu wapigane