Rashford Akerwa na Ubaguzi

Marcus Rashford, mshambuliaji wa Klabu ya Manchester United amesema kuwa anatambua kwamba ana rangi nyeusi anaifurahia rangi hiyo wale wanaombagua hawatendi jambo la haki na wala wasifikiri kwamba atawajibu.

Nyota huyo wa Manchester United alikutana na jambo hilo kupitia mitandao ya kijamii muda mfupi baada ya timu yake kulazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Klabu ya Arsenal, Uwanja wa Emirates kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram mashabiki walianza kumshambulia Rashford kwa kutumia emoji za nyani na wengine waliweka ujumbe kwamba anapaswa kwenda maeneo ya makazi ya wanyama jambo ambalo limemuumiza nyota huyo kuhusu ubaguzi wa rangi.

Mbali na Rashford mwenye miaka 23 pia suala hilo la ubaguzi wa rangi lilimtokea nyota mwenzake Axel Tuanzebe na Anthony Martial pia nyota wa Chelsea Reece James na nyota wa Klabu ya West Broms Romaine Sawyer nao pia walikutana na ubaguzi kwenye mitandao ya kijamii.

Rashford kupitia tweet amesema:”Utu na mitandao ya kijamii umekuwa kwenye wakati mbaya kwa sasa. Ndio ninajua kwamba mimi ni mweusi na ninaishi na katika hilo ninajivunia kabisa kwa rangi ambayo ninayo.

“Hapana, hapana, ujumbe wowote ambao utauandika hapa ama hakuna mtu yoyote yule ambaye anaweza kunifanya nijiskie tofauti.

“Samahani ikiwa unahitaji kuona ninaweza kuchukulia tofauti hilo haliwezi kutokea kwangukiwepesi tu hautaona kwangu samahani. Kuna watoto wazuri ambao wanaipenda rangi yangu na wanafuata ndoto zao siwezi kuwaangusha,”.


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

13 Komentara

    Ubaguzi sio Jambo jema linakera kabisa

    Jibu

    Kwenye game ubanguzi wa rangi hautakiwi

    Jibu

    Rashford amesema kweli
    Ila ubaguzi sio mzuri kabisa wabadilike wawe wazungu kama jina lao

    Jibu

    Huu ubaguzi sijui utakwisha lini? Hayo mambo yanawatesa sana waafrica wanaochezea club za ulaya

    Jibu

    Ubaguzi mbaya sana.yn unatakiwa kukomeshwa

    Jibu

    Ubaguzi sio kitu kizuri

    Jibu

    Ubaguzi sio poa

    Jibu

    Nikweli ubaguzi sio kitu kizuri

    Jibu

    Hiki ktu akpendez kabsaa

    Jibu

    Rashford yupo sahihi anyamaze tu kimya ila ubaguzi haufai kwenye soka

    Jibu

    Kwenye soka ubaguzi hautakiwi

    Jibu

    Ubaguzi sio mzuli

    Jibu

    Rashid hapendi kabisa masuala ya ubaguzi

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.