Jahazi linaendelea kuzama linapokuja suala la Liverpool kutetea ubingwa wa EPL msimu huu. Hii ni baada ya kupoteza mchezo wa 3 wakiwa Anfield.
Mabingwa wa tetezi wa EPL wamejikuta wakiambulia kipigo kizito cha magoli 4-1 kutoka kwa Manchester City jana usiku.
Mengi yamesemwa baada ya mchezo huu, lakini la Roy Keane limekuwa na maono tofauti. Keane ambaye amekuwa akichambua mienendo ya timu mbalimbali, anaiona Liverpool ikirudi ilipotoka.
“Kwangu ni mabingwa wabaya. Utasema huu ni msimu wa kipekee, ni Corona. Lakini sio sababu, nyie ni mabingwa watetezi, nyie ni Liverpool.

“Endeleeni kucheza hivi na mtakaa miaka mingine 30 bila kombe.” alisema Roy Keane baada ya mchezo dhidi ya City.
Kocha Jurgen Klopp amekuwa ni mwenye kutafuta sababu kwa kila mchezo anaocheza msimu huu. Kwa hali ilivyo sasa hivi, majogoo ya Uingereza yanapungufu ya pointi 27 wakilinganishwa na walivyokuwa muda kama huu msimu uliopita.
Hii ni kusema kuwa Klopp na vijana wake hawana jipya msimu huu au ni wapi hasa wanaelekea?
Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.



warda
Liverpool bado wanafuraha ya ubigwa ndo mana wanapoteza sana
Magdalena
Liverpool msimu huu waandike maumivu
Khadija
Livepool msimu huu wameula wa chuya
Venerose
Liverpool wanatakiwa wafanye kazi ya ziada
Rahma
Liverpool wanakazi nzito wanatakiwa wapambane
Hopemwaikuka
🤣🤣🤣🤣
Dorophina
Liverpool walikuwa na kibarua kizito sana jana
Angelina
Liverpool hawako sawa
Ernest Kimeru
Mpira hasa EPL kumekuwa na changamoto sana maana kila timu imejipanga kisawasawa japokuwa kuna mapungufu madogo madogo, Muda umefika kwa Klopp na vijana wake kujaribu kurudi kwenye mbio za ubingwa, Squard rotation inahusika kwa Liverpool japokuwa kwa upande mwingine ni jambo gumu sana kulifanya kwa wakati ambao unahitaji ushindi
Sania
Liverpool wanayumba
Mwanahamisi
Liverpool win
lombo
well
Sarah
Liverpool hawaii sawa
Lydia Emmanuel Magoti
Liverpool Wana kwama wapi sasa
Ester mmakasa
Jamani Liverpool wanatuangusha sana
Sylvester
Inawezekana ikawa kweli kwani naona wchezaji wengi bora kama Salah wataondoka pale