Kocha wa Bayern Munich Hans Flick anatarajiwa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na timu ya taifa ya Ujerumani huku akirithi mikoba ya Joachim Low.
Akiwa na Bayern Munich Flick alifanikiwa kuchukua makombe 6 akiwa na klabu kwa kipindi cha miezi 18 tu! Hans ataondoka klabuni hapo akiwa na kumbukumbu mbaya ya kushindwa kutetea taji la UEFA msimu huu baada ya kuondolewa na PSG jana usiku kwa jumla ya magoli 3-3.
Flick atachukua nafasi ya Jorgi Low ambaye ameomba kuacha kazi ya kufundisha timu ya Ujerumani baada ya mashindano ya EURO 2020. Ujerumani imekuwa ikiwaajiri makocha wazawa kufanya kazi hiyo. Na kwa kiwango kikubwa makocha hao huwa wanafanya kazi kubwa sana.
Joachim Low alichukua timu ya ujerumani kwa muda wa miaka na akafanikiwa kuchukua makombe akiwa na Ujerumani, miongoni mwa makombe aliyochukua ni Kombe la dunia la mwaka 2014 kule Brazil. Kuondoka kwa Low katika timu ya taifa kunahusishwa na kuchukua nafasi ya kocha wa Real Madrid, Zidane endapo atashindwa kuchukua ubingwa wa UEFA au La Liga.
Je, Flick atendeleza kufanya makubwa na timu ya taifa kama alivyofanya na Bayern Munich au itakuwa changamoto kubwa zaidi?
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



Venerose
Hongera sana HANS
Sarah
Ongera sana Hansi
Adelta
Flick yuko vizuri
warda
Safi sana bonge la shavu