Pavol Kutua Mamelodi Sundowns

Club ya Sepsi OSK ya Romania imeripotiwa kukubali ofa ya Euro 700,000 (Tsh Bilioni 1.9) kutoka Club ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ili imuachie Pavol Safranko (26) ajiunge nao.

Pavol
Sepsi OSK

Mshambuliaji huyo Pavol ambaye ni Raia wa Slovakia amefunga magoli 7, assist 4 katika michezo 25 akiwa na Sepsi OSK huku usajili huo ukitajwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya Club hiyo ya Ligi Kuu Romania.

Pavol amewahi kucheza Timu ya Taifa ya Slovakia akicheza jumla ya mechi 10, habari hii inakuwa kubwa Afrika sababu ni nadra sana Wachezaji wanaocheza Ligi Kubwa Ulaya au Bara la America kuja Afrika ila Mamelodi wameanza kuonesha njia kwa kuwaleta watu kama Gaston Sirino kutokea Uruguay na kuonesha uwezo mkubwa.

Pavol
Gaston Sirino

Ukiangalia katika viwango vya soka duniani vya FIFA, Taifa la Slovakia analotokea Pavol liko nafasi ya 36 kwa ubora huku Romania anakocheza wako nafasi ya 43 kidunia na anakuja Afrika Kusini katika Taifa lililo nafasi ya 75 hivyo inatafsirila kama dalili njema kwa Soka la Afrika kuleta wachezaji wa viwango.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Pavol yuko makini Sana

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Asanteni kwa makala

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    pavol yuko poa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.