Beki tegemezi wa pembeni ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar, Hassan Kessy amesema kuwa yupo tayari kusaini kwenye timu yoyote ambayo itahitaji saini yake hata wakiwa ni mabosi wake wa zamani, Yanga.

“Mimi ni mchezaji na nipo tayari kucheza popote kikubwa ni maslahi pamoja na makubaliano hivyo hata ikiwa ni Yanga sina tatizo nao mimi nitacheza.
“Kwa sasa nipo hapa Mtibwa Sugar na tunazidi kupambana ili kupata matokeo chanya kwani kila mechi inakuja tofauti na tunaamini kwamba tutapata matokeo kwenye mechi zetu zijazo,” amesema Kessy.

Nyota huyo alikuwa anatajwa kujiunga na Yanga kabla ya kuibukia Mtibwa Sugar akitokea Zambia ila mambo yalibadilika akaibuka Mtibwa Sugar.
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



Adelta
Popote kambi kikubwa maslai tu
Venerose
Safi sana kwa maamuzi yake
Sarah
Safi sana
warda
Hata wamchukue nani kipigo kipo pale pale